Mlingoti unaoshikilia Kibao kinachoonyesha mtaa wa Harden Ct,ukiwa umeanguka barabarani baada ya tufani ya IRENE kupita usiku wa kuamkia leo Aug 28,2011,huu mtaa upo Baltimore,Maryland
Hapa ni miti iliyoanguka,Baltimore,Maryland baada ya tufani ya IRENE kupita
Maeneo mengi ya DMV hayana umeme wala Cable hazifanyi kazi hii ni baada ya Tufani ya IRENE ilipopita maeneo haya mida ya 12:30 am mvua na upepo mkali uliokua ukienda 80 M/H(120 KM/H) ambao umeangusha miti mbali mbali ikiwemo miti ya umeme.
Sehemu nyingi miti imeanguka katikati ya barabara na zimekua hazipitiki
Wafanyakazi wakiendelea na kazi ya kuondoa miti iliyoanguka Barabarani,kama walivyokutwa na Camera ya VIJIMAMBO mitaa ya New Hampshire
Juu na chini sehemu kubwa ya Washington Metro Area taa za kuongozea magari hazifanyi kazi kwa hiyo unapoendesha jaribu kuwa muangalifu
Juu na chini zinaonyesha sehemu nyingi matatizo ni yale yale ya miti kuanguka na kutokua na umeme
No comments:
Post a Comment