Advertisements

Saturday, September 10, 2011

MAAFA YA KUZAMA KWA MELI YA ABIRIA -ZANZIBAR


AFRICAN UNION


union africaine



união africana


Mwakilishi wa Umoja wa Afrika (African Union) Balozi Amina Salum Ali kwa niaba ya Umoja wa Afrika nchini Marekani, anaungana na Watanzania wote popote duniani, kuomboleza kutokana na maafa ya Watanzania wenzetu yaliyosababishwa na kuzama kwa meli ya Spice Islanders usiku wa kuamkia leo katika mkondo wa Nungwi, Kaskazini mwa kisiwa cha Unguja. Aidha, Balozi Amina Salum Ali anawapa pole wale wote waliofikwa na msiba huu mkubwa na kumwomba Mungu awafariji wale wote waliofikwa na tukio hili la kusikitisha.
Mwenyezi Mungu andelee kuwapa unafuu wa kiafya wale waliojeruhiwa katika tukio hili na pia azilaze roho za wale wote waliopoteza maisha yao mahali pema peponi, Amina.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.

No comments: