Advertisements

Saturday, September 10, 2011

Salamu za Rambi Rambi

Jumuiya ya Watanzania waishio New York na vitongoji vyake inatoa salamu za rambi rambi kwa wale wote waliofiwa au kupoteza ndugu na jamaa katika ajali mbaya ya kuzama kwa feri iliyokuwa ikielekea Pemba jana usiku. Vile vile tunawapa pole wale wote waliopata majeraha mbali mbali katika ajali hii.

Tunaomba Mwenyezi Mungu aziweke mahali pema peponi roho za wote waliopoteza maisha yao.

Vincent L. Mughwai
NYTC-Secretary

No comments: