Habari za leo ndugu zangu watanzania, kunatabia mbaya sana imezuka hasa kwa dada zetu waishio ughaibuni(WASHINGTON METRO AREA).... tabia hii mbaya sijui niipe jina gani nadhani wengi wa akina dada hawa wamekuja Ughaibuni kibahati mbaya..... si kitu walichotegemea ndio maana wanakua hawana ustaarabu badala yake wana tabia za kutukanana kwenye kitabu cha uso(fb) bila aibu tena mitusi ya nguoni.
Hakuna binadamu mstaarabu ambae atajiona kwamba yeye ni bora kuliko mwingine, kwa mimi niliyefundishwa na wazazi wangu ambao walinipa misingi bora ya kuheshimu binadamu mwingine kama unavyojiheshimu wewe bila kujali tajiri wala masikini,mkubwa na mdogo kwamba binadamu wote ni sawa na hakuna binadamu mwenye roho mbili eti roho ya kwanza itachukua mitusi yako na roho ya pili itaendelea kua na raha.
Sasa nyie dada zangu mnao jiona bora kuliko wenzenu na kuanza kutukanana kwenye kitabu cha uso bila aibu mtafikiri mitoto wakati ni mimama mizima, bado mkaona kitabu cha uso hakitoshi; mkaamua kupeleka maugomvi yenu yasiyo na kichwa wala miguu na kuharibu sherehe za watu!!!...... hebu kaeni chini mfikirie kama hiyo sherehe ingekua yako ungejisikiaje?!, au hamfahamu kwamba sherehe kama hizi binadamu hufarahia mara moja katika maisha yake!!???, Je! baada ya kutia doa sherehe ya mwenzenu ulishathubutu hata kupiga simu kumuomba msamaha???? sidhani kama mna unastaarabu huo.
Nakuombeni sana dada zangu mkae chini mfikirie maisha ni mafupi sana, hujui kesho na keshokutwa utakua wapi na hujui huyo unaemtukana ndie atakae kusaidia kesho au la, chonde chonde dada zangu kaeni chini mtafakari.....hauna haja ya kujiita kwamba mimi ni mwislamu safi au mkristu safi wakati huwezi hata kusamehe tafadhali mrudieni Mungu wenu,Mwenyezi Mugu hadanganyiki,
Mwisho nawaombeeni kwa mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awajalie UPENDO kusudi muishi maisha yaliojaa AMANI na palipokua na giza Mungu apatie nuru,awape hekima ya kutambua mabaya na mazuri na awatie nguvu na ushujaa muweze kuswamehana AMINA!
NI MIMI MKEREKETWA.
18 comments:
hapo tena pabaya ndugu,siyo wamekuja kwa kubahatisha tu ndiyo ukweli wenyewe ukianza kutizama ilikuwaje utasikitika na mambo wanayoyafanya siyo wanawake tu hata wanaume pia,hivi niulize kwanza wanaume wanawake zenu,au marafiki zenu mnaotarajia baadaye kuwanao kimaisha wakiwa wanavituko kama hivi inakuwaje?tena unalikuta janaume linasema shauri zao hao wanatofauti zao bwana angalia hiyo itakula kwako siku moja kama haurekebishi tabia,nia aibu na kujivunjia heshima maana kwa sasa unaambiwa ukienda dmv uwe na mlinzi sasa hii ni sifa au?jamani tusitiane aibu pamoja hapa kila mtu kaja kivyake ustaarabu kitu cha maana tuonekane basi kama tumetoka kwa wazazi mzazi siyo lazima akuzae,mnatukana mpaka mama zenu akili hizo,ulimi kiungo kidogo tu lakini madhara yake makubwa basi tujichunge.tunajua kusemasema watu wengine wamejaliwa
The article was kind of interesting. Now,if you called youself an anonymous, how'd you know that people involved in an episode have not contacted the newly wedds and appologized. The political corectness could have cemented your argument much stronger had you chosen not to react emotionally and leble those ladies inappropriately. A positive article that did not question the motive behind coming to diaspora would appeal much better to those knuckleheads reather than treating them like thugs. Civilized readers cannot distinguish between yourself and people whom your message has been centered to.If you believe that other peoples' sins will make you a saint, you do not have to act like sinners by cursing sinfull people. Peace!
Kikubwa na cha maana inabidi watu wakue jamani,kwani haya maisha ya vita na maneno maneno kila siku vitaisha lini,na mtu anayesema anasemwa,na yeye pia lazima anasema watu,lakini cha maana watu inabidi mkue na mstaarabike kwani neno USTAARABU kwenu ni lugha ya kichina? Yaani sasa hivi DMV ndio inajulikana state ya kwanza kwa malumbano na majungu na ngumi juu na hasa kwa wanawake na ukija kuangalia chanzo cha ugomvi ni hakina maana kabisa,kama mnaona hamna la kufanya jaribuni hata kukaa chini mkatafakari zaidi kuhusu maisha kuliko kupigana majungu na matusi makali kama yale na plus kutaka kuharibu shughuli ya watu na jaribuni kuwa wastaarabu hata kwenye shughuli za watu otherwise mtakuwa WANTED kila shughuli
Jamani mnapoyatibuwa huko hamkumbuki kama mna mungu,hivi inakuwaje mmeisha vuana nguo ndiyo unajua kuna mungu ingekuwa,waume kwa wake muwe wastaarabu,watu wazima wenye watoto na wajukuu mnafanya mambo ya ajabu jamani ni aibu iliyoje na sababu zenyewe unakuta hasa wanawake mnagombania wanaume na wanaume wenyewe virukanjia au huyo mwanamke ukiesabiwa mduara aliocheza utashaa.mnafanya watu wote wanaokuja huku ughaibuni hasa usa,uk,kuonekana wahuni tu,fanyeni maendeleo nyumbani siyo kutambishiana nguo na magari akili hizo na rent zinawashinda ishini maisha ya amani ukiangalia wote mazabe matupu hata kama vitu mnavyo ni zabe tu
afadhali mdau umesema maana mie hili jambo liliniboa. mijanamke mizima inakaa inagombana kwa sababu za kijinga and as if it is not enough wakayaendeleza facebook. yall should be ashamed of yourself! you should worried how to get makaratasi na mambo ya muhimu mambo ya ngumi mlitakiwa myaache mara mlipoingia kwa ndege kuja majuu. jamani hii ni majuu siyo uswahilini, can't you tell the difference!
sipendi kweli watu wanaotukania wazazi. ni akina nani hao tuambieni tuweke majina yao kwenye "do not call list"
UKIMWI TU!
It doesn’t matter whether they apologized to the newly weds or not, kile kitendo cha kupigana kilitia doa kubwa sana kwenye shughuli ya watu PERIOD! Na ukiangalia source ya ugomvi eti ni wanaume tena ma-boyfriend tu, kha aibu!
Amen to all the ppl who have voiced their opinion. If you have a friend using profanity on FB please delete them as they reflect on YOU. This is a shameful uniqueness like the article says most of those ppl are trying to bring their complicated life to other ppl who have uncomplicated life. Hawa wasichana lazima wakue sasa kila wakati maneno na unafiki mwingi na majungu. Elimu hawana, maisha yao ovyo ovyo kutwa maneno tu ya kusema na kuchunguza watu wanaishi vipi na kujifanya wanazo wakati kazi zao kuosha mabibi. Kuoa au kuolewa does not mean kama wewe ni zaidi au una furaha wengi wenu ni majuha tu kama brotherman anaevuta aspen. Wasichana wengi wa DMV nendeni shule au piga boksi hata tatu kama huna kitu cha kufanya saidia ndugu zenu. Acheni uhuni na maneno wakati mna madeni kibao na matatizo kibao kwenye maisha yenu. Jitahidini kufanya kazi muwe na maendeleo kwani kutambiana na kubezana hakuna tija kwani watu walioendelea mazungumzo yao huwa juu ya vitu vya maendeleo na wale wasio na maendeleo mazungumzo yao ni juu ya watu. Mwl Nyerere alisema umaskini wa mawazo ni umaskini mkubwa kupita wote kabisa. Kila mkiona shughuli mnakimbilia madukani kushoplift ili muonekana na designer cloth. Acheni utoto na mjiheshimu. Wengine mnafikiri thighs and butts will get you somewhere. It is time now for the ladies to mean something more than thighs and butts.
Mpilipili
1600 Pennysylvania ave.
mpilipili nimeipenda hiyo ya 1600....nitakubip
Lack of elimu, we kama una muda wa kuandika mambo kama gazeti fb kweli kazi na elimu huna!! Mnatia aibu kinoma yani, kuonyeshana magari, nguo mnazovaa, viatu, n.k. unataka viashirie nini haswa? I swear to God ni ushamba na ulimukeni wa hali ya juu! Wapumbavu woteeeee!! Na hao wanaume waliowaoa nao ni mazezeta tu Ku....ae zao!!
i know ni ulimbukeni uliopindukia. if u grew up with those things huwezi kuvipapatikia ukubwani. someni shule walau mpunguze viazi humo vichwani mwenu! tafuteni walau papers basi maana mbona hatuwasikii mkijisifia mmeenda kutembea Tanzania toka mmekuja!
Nakubaliana kabisa matusi hapa DMV hayajaanza leo yapo from HI5 mpaka facebook! What a shame wanawake na si wasichana wasio na haya kutoa kauli chafu kutamka sehemu za siri kama zilivyo???? What a shame? Hawa watu ni malimbukeni wametoka uswahili kwenye vyoo vya shimo kufika marekani kwenye maflat na vyoo vya kuvuta they lost their mind. U need to loose half of ur brain or be so uncevilized to act like them! Puuuu na hao wanaume wanaotembea nao kazi mnayo. Nimekaa marekani over 20yrs na siwezi hata kutamka tusi moja la kizungu lakini ukiwasikia wanavyoongea utadhani walizaliwa huku, dirty mouths! Someni Hi5 na facebook u will be shocked! I was waiting for somebody to start this topic DMV kunaharibika we were cool in 80's and early 90. Ndiyo maana nimeacha kwenda kwenye shughuli ya mtu yeyote except misiba cha kutolewa jicho nini?
hahahahah vyoo vya shimo, na mie nishaisikia hiyo. sasa leo hii badala ya kwenda kujenga vyoo vya kuvuta huko makwao wanabaki wanashindana matusi kuona nani ana mdomo mchafu zaidi. nafikiri hiyo midomo michafu ni athari ya vyoo vya shimo walivyokuwa wanatumia huko makwao chembechembe za "vitu fulani" zikawa zinarukia midomoni! watu wanatukana matusi utadhani wamesomea, ni aibu!
halafu eti wanajiita "classy".....obvious they don't even know the definition of classy. classy people don't fight in public, "gheto" people do. yaani mimi hii kitu imeniboa sana! naona hata aibu kuwaambia watu nakaa DC ah!
jamani nimewasikia ngoja nijifungue kwanza sitaki headach bure humu,
Kuna msemo unasema hata ukimlisha chakula ya aina gani mbwa lakini akienda haja kubwa, kinyesi ni cheusi. So i guess these fools they are in wrong place warudi kariakoo wakafanye huo upuuzi na si hapa shenzy type
Wamezidi jamani dc toka miaka ya nyuma,maneno na dharau hapa ni kwao ukiangalia watu wenyewe utafikiri wauza baa nadhani mnakumbuka nyumbani kule wauzaa bar walivyo kosa heshima wale ndiyo wanafanya chochote na kusema chchote kibaya,wamekaa usoni utafikiri sijui nisemeje,ustaarabu kitu cha bure jamani,luke tunakushukuru sana sisi wote ni ndugu kama usemavyo katika jamii hii leo kwangu kesho kwa mwingine msemo huu siyo wa msiba tu ukiuangalia kwa undani utaelewa ni nini jamani acheni watu wawasifie siyo mjisifu dc fun kweli
Post a Comment