Kwa ndugu Watanzania wenzetu
Kwa niaba ya Watanzania waishio nje ya nchi, DICOTA inachukua fursa hii ukiwa ni wakati mgumu kwa Taifa letu na kwa wananchi wote wa Tanzania hususani kwa ndugu jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao katika ajali ya meli MV Spice Islander.
DICOTA, tumepokea huu msiba kwa mshtuko na majonzi makubwa. Tunatambua kwa hakika kuwa hiki ni kipindi kigumu kwa wafiwa na Taifa letu kwa ujumla. Pamoja na umbali wetu tunapenda kuwahakikishia ndugu zetu kwamba tuko pamoja nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa kwa taifa letu.

Kwa wale waliopata majeraha, lakini maisha yao yakasalimika tunapenda kuwapa pole sana na Mwenyezi Mungu awaponye haraka ili muweze kurudi katika afya zenu za kawaida na kuweza kuungana na familia na ndugu zenu katika kulijenga Taifa letu.
Tunapenda kuchukua nafasi hii pia kuwashukuru Viongozi wa Serikali, Mashirika ya kiserikali na yasio ya kiserikali, watu mmoja mmoja na taasisi zote kwa juhudi zao za kuokoa maisha ya wenzetu.
Mwisho tunapenda kutoa changamoto kwa jumuiya zote duniani kuona ni kwa namna gani tutaweza kuwasaidia hawa wenzetu, sasa na hata baada ya hali ya kuokoa maisha ikiwa imetulia.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu wabariki watu wa Tanzania na atuwezeshe kukipita kipindi hiki kigumu tukiwa na mshikamano ulio imara kama Taifa.
Uongozi wa DICOTA (Diaspora Council of Tanzanians in America)
No comments:
Post a Comment