
Hii picha ilitoka kwenye gazeti la Daily News enzi hizo miaka ya 70 huu ulikua uwanja wa kumbukumbu ya Karume,Ilala,Je unaweza kuwakumbuka wachezaji hawa hii ilikuwa mechi ya Simba na Yanga
----------------------------------------------------------------------------------------------
----------------------------------------------------------------------------------------------
Za leo Dj
Naomba ufanye sahihisho kidogo katika maelezo ya hiyo flashback.Mechi hiyo ilichezwa uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. Na siyo uwanja wa Karume.Kwa kumbukumbu zangu Mechi hiyo ilichezwa mwezi juni 1974.Wanaoonekana pichani ni Golkipa wa Simba Athumani Mambosasa (RIP)
Mshambuliaji hatari wa Yanga Kitwana Manara na Beki nambari 2 wa Simba Shabani Baraza.Katika mechi hiyo Yanga iliishinda Simba kwa mabao 2-1.na kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara.
Simba ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Abasi Dilunga. Yanga ikasawazisha dakika za majeruhi kupitia Mshambuliaji wake mwenye mashuti makali Gibson Sembuli (RIP) Kwenye muda wa nyongeza Sunday Manara akaipatia Yanga bao la ushindi. tukio moja la ajabu lililotokea katika mechi hiyo ya watani wa jadi. Mshambuliaji hatari wa Simba aliyejulikana kwa jina la Saad Ali alitupiwa Jini uwanjani na kuanguka na hatimaye kupoteza fahamu.Na huo ndio ukawa mwisho wa his young football carreer
Ok Dj Salam zao Capitali.
Mdau professeur Mrisho
1 comment:
Samahani sana kuingilia kwenye marekebisho yako,kuhusu wachezaji kwenye picha ni sawa kabisa lakini goli la simba lilifungwa na adam sabu aliyeingia badala ya Saad ali ambaye alipoteza fahamu uwanjani.
Post a Comment