ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 7, 2011

HAPA NA PALE KATIKA PICHA

Msanii Faida Makame Shaali, akiwaongoza wachezaji wenzake katika ngoma inayojulikana kama 'Kubwaya' wakati wa sherehe za maridhiano na Umoja wa Kitaifa visiwani Zanzibar zilizoandaliwa na Taasisi ya Swahili Center, juzi katika Kijiji cha Nungwi, Unguja kwa kushirikiana na ubalozi wa Norway.(Na Mpigapicha Wetu).
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya (aliyebeba mkoba), akicheza ngoma na kinamama wa mkoa wa Ruvuma, walipompokea mjini Songea juzi. (Picha na Muhidin Amri)
Wasanii wa kikundi cha ngoma za asili cha Egumba, kilichoko Wilaya ya Musoma Vijijini, wakicheza ngoma ya Rhitungu, wakati wa mkusanyiko wa kusherehekea miaka 50 ya Uhuru mjini Musoma hivi karibuni. (Na Mpigapicha Wetu)

Picha zote kwa hisani ya Majira

No comments: