Galinoma alifariki dunia jana asubuhi wakati akikimbizwa katika Hospitali teule ya Wilaya ya Iringa Vijijini ya Ipamba.
Mtoto wake, Magreth Galinoma, alithibitsia baba yake kufariki dunia jana asubuhi kwenye gari wakati akikimbizwa katika hospitali hiyo kwa matibabu kutokea jimboni mwake.
Alisema kabla ya kifo chake, baba yake alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo.
Naibu Spika, Job Ndugai, alithibitisha jana kutokea kwa kifo hicho alipozungumza na NIPASHE kwa njia ya simu.
Galinoma alikuwa mbunge wa jimbo hilo kuanzia mwaka 2005 hadi 2010 alipostaafu.
Nafasi yake imechukuliwa na Mbunge Dk. Wiliam Mgimwa, wa CCM baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Oktoba mwaka 2010.
Kabla ya mauti hayo kumfika, Galinoma aliwahi kupelekwa nchini India kwa matibabu kwa muda wa wiki sita.
Galinoma alikuwa mtumishi wa serikali mstaafu aliyeshika nafasi mbalimbali wakati wa uhai wake.
Miongoni mwa nafasi hizo ni pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mbuga za Wanyamapori, Mwenyekiti wa Bodi ya Mashirika ya Umma (Scopo, Katibu wa Tume ya Uchunguzi wa viongozi.
Ameacha watoto na wajukuu kadhaa. Miongoni mwa watoto wake ni mwanamuziki Innocent na Buti Jiwe maarufu kama Enry Galinoma.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment