Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT) jijini Dar es Salaam kipo katika mchakato wa kuondolewa na badala yake vitajengwa vituo vitatu vya kuwahudumia wasafiri kutoka mikoani na nje ya nchi.
Akizungumza wakati akikagua kituo cha mabasi yaendayo mikoa ya kusini, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki, alisema hatua hiyo inachukuliwa ili kuondoa msongamano wa magari katikati ya jiji.
Alisema mkakati huo unachukuliwa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa baada ya kubaini kituo hicho kinasababisha msongamano wakati wa uingiaji na kutoka kwa mabasi.
Sadiki alisema baada ya kuondolewa kituo hicho kitageuzwa kwa kituo kikuu ya mabasi yaendayo kasi, ambapo mradi wake unaendelea kufanyiwa kazi.
Alitaja maeneo yakayojengwa vituo hivyo kuwa ni Mbezi kitakachopokea magari kutoka Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na Magharibi ya nchi, Tegeta kinakachotoa huduma kwa Mikoa ya Kaskazini na Mbagala kwa magari ya Mikoa ya Kusini.
"Tumeona tutekeleze mpango huu kwa ajili ya kupunguza msongamano wa magari katikati ya jiji," alisema Sadick.
Aidha, aliingeza Jumuiya ya Umakuta inayomiliki kituo hicho kwa hatua yao ya kutenga eneo hilo kwa ajili ya kuyaruhusu magari yanayokwenda kwenye mikoa hiyo kukitumia kwa ajili ya wateja wao.
"Tunawapongeza kwa kuchukua hatua hii kabla ya sisi kuanza kutekeleza mpango wetu, nawaombeni endeleeni kukiboresha kituo ili kiweze kuendana na ubora unaotakiwa," alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Awali kwenye risala ya Umakuta, ileleza kituo hicho kilichoanza mwaka 209 moaka sasa kinahudumia mabasi 20 kwa siku pamoja na daladala zinazokwenda sehemu mbalimbali jijini.
Ilieleza kutokana na uwepo wake jumla ya watu 120 wamepata ajira ndani ya kituo hicho, lakini bado kinakabiliwa na matatizo ya kukosa mapato ya kutosha kutokana na kutokuwepo na miundombinu ya uhakika itakayofanya kituo kitoe huduma kwa vipindi vyote vya mwaka.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment