ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 12, 2012

Mapinduzi ya Zanzibar kutimiza miaka 48 leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein, leo anatarajia kuwaongoza mamia ya wananchi wa Zanzibar katika maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kilele cha maadhimisho hayo kinatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Amani ambaps Dk. Shein atapokea maadamano ya wananchi kutoka mikoa mitano ya Zanzibar kabla ya kupokea heshima na kukagua vikosi vya ulinzi na usalama.

 Maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi yalizinduliwa Januari 2, mwaka huu, ambapo viongozi mbali mbali wa kitaifa walizindua miradi ya maendeleo katika sekta za uvuvi, mawasiliano, ujenzi wa majengo ya serikali na uwekaji wa mawe ya msingi ya ujenzi wa shule za sekondari 16 Zanzibar.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed, alisema kwamba matayalisho yote ya maadhimisho hayo yamekamilika.
CHANZO: NIPASHE

No comments: