ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 9, 2012

NEWS ALERT: Msanii Diamond ahukumiwa kwenda jela miezi sita ama faini shilingi elfu 50 kwa kumpiga mwandishi iringa

Mwanamuziki Diamond na madansa wake wakiwa katila mlango wa Mahakama ya Iringa leo asubuhi kabla ya kupanda kizimbani kujibu mashtaka ya kumshambulia mwana habari Francis Godwin. Msanii huyo na madansa wake walikiri kosa na hakimu akawahukumu kwenda jela miezi sita ama kulipa faini ya shilingi 50,000/- kila mmoja, na kuamuru mwanahabari Francis Godwin alipwe fidia ya shilingi 90,000/-.

Habari toka mahakamani hapo zinasema Diamond na madansa wake wamelipa faini na kauchiwa huru, ila mwanahabari Francis Godwin amegoma kuchukua fidia ya shilingi 90,000/- na anatarajia kufungua kesi ya madai dhidi ya Diamond na kudai fidia ya kudhalilishwa, kupigwa na kupotezewa zana zake za kazi kwenye mahakama ya Wilaya.

"Tayari nimeshaongea na mawakili wangu na wanakamilisha taratibu za kumrudisha kizimbani tena Diamond
 kwa kesi ya madai". Francis Godwin kaiambia Globu ya Jamii sasa hivi kwa simu, na kuongezea kwamba anashukuru kwamba heshima imewekwa japo haki ya dhamani yake kama binadamu na vifaa haijatendeka

5 comments:

Anonymous said...

Jamani Bongo acheni ujinga, faini ya nini tena? Hawa wasanii feki (fleva artists) lazima wakomeshwe. Kumpiga mtu na kumzalilisha hadharani kisa wewe ni mbangaizaji wa fleva is an insult na lazima huyu kijana na wenzake wakomeshwe kwa kwenda jela si chini ya miaka miwili. Wakitoka huko watarudi na ustaarab na kuachana kabisa na mambo ya kuiga iga (kuimba fleva) na kurudia kazi zao za zamani za kuuza maji ya chupa. Nawasilishaa!

Anonymous said...

we uliyesema hayo yote hapo juu kwani hujui siku hizi bongo kuna maselebrity?? hata kama hawana mapesa ila wanajuliakana tu.....

Diamond jaribu kufanya vitu vinavyoenda na umri wako mambo ya kupigana yashapitwa na wakati... binafsi ni mpenzi sana wa nyimbo zako haswa "NALIA NA MENGI" lakini sikufichi kwa haya mambo yako utanipoteza nikiwa kama shabiki wako, naomba uwe mtu wa heshima pls

Anonymous said...

Mie namtetea wanamtafutia sababu tu aebde jela wamkomeshe hao waandishi wa habari wamezidi kumfatilia maisha yake mtu hadi achukue uamuzi wa kukupiga inamaana umevuka,mpaka kumuuliza maswali ya kijinga wamemfanya chambo kila siku kumzushia ktk magazeti yao ya umbeya.

Waandishi mjifunze taaluma yenu kuandika ya kweli nasio kuzushia watu ili mradi muuze magazeyi yenu .mnadhalilisha watu na kuwadumaza kiakili mkipigwa mnakimbilia mmahakamanu

Anonymous said...

We mtangazi wa clouds hapo juu acha ujinga wako, toka lini waimbaji wa karaoke wakawa macelebrity? Ni ninyi clouds radio ndio mnawapa ujiko hawa feki artists na kujiona ni wanamuziki kweli kumbe mavi tu. Huyu yanki lazima ashikishwe adabu kama vile TID miaka ya nyuma.

Anonymous said...

let them grow up hawa bado utoto unawasumbua na siyo kosa lao kwa sasa ni watu wa kuonewa huruma