ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 19, 2012

Sekondari yakosa wanafunzi

Mkuu wa Mkoa wa Iringa,
Dk. Christine Ishengoma



Wanafunzi zaidi ya  200 waliomaliza darasa la saba mwaka jana na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari ya Kata ya Manda, Wilaya ya Ludewa mkoani Iringa, wamekacha masomo baada ya kushindwa kuripoti shuleni.
 Hadi sasa ni wanafunzi watatu walioripoti shuleni licha ya uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo kupiga kelele mara kwa mara kuhusina na mwamko wa elimu wilayani humo.
 Hayo yalibainika juzi a baada ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, kufika katika wilaya hiyo kwa lengo la kujitambulisha kwa wananchi tangu alipoteuliwa  kuwa mkuu mpya wa mkoa huo.
 Katika ziara hiyo, Dk. Ishengoma alishtuka kukuta shule hiyo ikiwa imepokea wanafunzi watatu tu kati ya 200 ambao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza huku viongozi wa Halamshauri hiyo wakiwa hawana majibu sahihi.

 “Mimi nashangaa viongozi mnafanya nini maana watoto zaidi ya 200 hwajaripoti hadi hivi sasa ni balaa, natoa wito hakikisheni wanafunzi hawa wanapatikana mara moja na wanaanza masomo,” aliagiza.
CHANZO: NIPASHE

No comments: