ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 21, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

BOXING FEDERATION OF TANZANIA (BFT)
                                                                           SLP 15558
                                                                                              DAR ES SALAAM
                                                                                     Email;bft.tanzania2009@gmail.com
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

     KOZI YA YA KIMATAIFA YA KUFUNDISHA MCHEZO WA NGUMI

Kozi ya Makocha wa Ngumi inayoendelea Kibaha, Pwani katika shule ya Filbart Bayi, inaendelea vema chini ya mkufunzi aliyeletwa na Chama cha Ngumi cha Dunia (AIBA) Ndg Josef Diouf kutoka Senegal.

Ikiwa imefika siku ya sita makocha wanaohudhuria  mafunzo hayo ya siku kumi, wamelizika na kiwango cha mkufunzi huyo kwa kusema kuwa mbinu za kiufundi na ujanja wa  ufundishaji wa mchezo wa ngumi anazo wafundisha ni za kisasa na kwamba kwa sasa wameelewa msingi wa ufundishaji,hasa kwa kumwanzisha, kumwendeleza mchezaji hadi kufikia kuwa mchezaji wa kimataifa toufauti na awali ambapo walikuwa wanafundisha kwa mazoea bila kuwa na mbinu za kuwafanya wachezaji ili kuleta upinzani hasa katika mashindano ya kimataifa.
Lakini pia wamejifunza namna ya kuandaa ratiba za ufundishaji za siku kwa siku ,wiki,mwezi na ratiba ya mashindano yanayowakabili
Kwa kujigamba Makocha kutoka mikoani wamesema ujuzi wao wataanza kuonyesha katika mashindano ya Taifa yatakayofanyika katikati ya mwezi wa February ya kuwa  kutakuwa na ushindani mkali sana hasa kwa kuzingatia mikoa mingi makocha wake wamepata mafunzo hayo,na sasa timu za vyombo vya ulinzi na usalama  na zile za Dar es salaam ziwe tayari kupata upinzani wa hali ya juu kwa kuwa sasa hata vilabu vya kutoka mikoani pia  zina mbinu na ujanja wa ufundishaji kulingana na mabadiliko ya mchezo wa Ngumi Duniani.
Kozi hiyo inatazamiwa kumalizika tarehe 24/01/2012 na walimu watakaokuwa wamefaulu watatunukiwa vyeti vya kimataifa vya daraja la kwanza(level 1) na kuingizwa katika Database za Chama cha Ngumi cha Dunia AIBA na kwamba watakuwana haki ya kufundisha mchezo wa Ngumi popote Duniani

Wakati huo BFT kwa masikitiko makubwa inasikitika kupatwa na msiba wa bondia wa timu ya Taifa Godfrey Mbunda aliyefariki kwa kugongwa na gari wakati yeye akiwa anaendesha pikipiki maeneo ya mbezi.ni pigo kubwa katika medani ya mchezo wa ngumi kwa kuwa bado mchango wake ulikuwa unahitajika kwa suala la maendeleo ya mchezo wa ngumi Tanzania

Makore Mashaga
KATIBU MKUU
                         MOB. 0713 588818 

No comments: