Kumbuka ndoa ni tendo la heri, hivyo shetani naye hutumia nafasi hiyo kuwaharibia! Kumuingiza Mungu katika uhusiano wenu kuna maana, mtakuwa katika ulinzi wenye nguvu zaidi.
TABASAMU lako ndiyo ishara kwamba upo tayari kwa ajili ya somo linaloendelea hapa katika All About Love. Marafiki zangu, kukunja uso ni tatizo, furaha ni tiba. Tafuta kufurahi mara nyingi kadiri uwezavyo ili kukuongezea siku zako kuishi hapa duniani.
TABASAMU lako ndiyo ishara kwamba upo tayari kwa ajili ya somo linaloendelea hapa katika All About Love. Marafiki zangu, kukunja uso ni tatizo, furaha ni tiba. Tafuta kufurahi mara nyingi kadiri uwezavyo ili kukuongezea siku zako kuishi hapa duniani.
Yes! Ndivyo wataalam wanavyosema, tabasamu lako linakuongezea muda zaidi wa kuendelea kuwa chini ya uso wa dunia, huzuni ni ishara ya kupunguza umri wa uhai wako.
Ndugu zangu, tupo kwenye msimu wa Sikukuu ya Wapendanao ambayo kwa Kiingereza inajulikana kama Valentine’s Day. Nilipaswa kuzungumza machache nanyi kuhusu siku hii, lakini kwa sababu tayari kuna somo jipya linaendelea, nimeshindwa kufanya hivyo.
Hata hivyo, si neno, kwa kutambua uhitaji huo, funua ukurasa wa saba wa gazeti hili, zipo dondoo chache za kukufanya uifurahie siku hiyo. Marafiki zangu kwa mada kwa ujumla wake juu ya siku hiyo muhimu kwa wapenzi usikose nakala yako ya gazeti la Ijumaa.
Ukinunua gazeti hilo, nenda moja kwa moja ukurasa wa kumi utakutana na safu ya Lets Talk About Love, hapo utapata elimu kikamilifu juu ya Valentine’s Day.
Turudi kwenye somo letu, bado tupo kwenye mfululizo wa mada inayohusu siri 20 za kufurahia mapenzi. Wiki iliyopita niliishia kwenye siri ya saba, sasa twende katika siri nyingine zinazoendelea.
8. MFANYE NAMBA MOJA
Kuna baadhi ya marafiki wana fikra potofu (hasa wanaume). Hawa wanaamini kumpa mwanamke nafasi katika maisha ni kumfanya akukalie. Si kweli. Mwanamke unapompa nafasi ya kwanza, anaufurahia uhusiano wenu.
Anajiona mwenye hadhi kubwa zaidi kwako, hutafuta njia za kukufanya umpende maradufu, kuliko kumuacha akijiona hana nafasi.
Ongozana na mpenzi wako kwenye kumbi za burudani, mialiko ya sherehe mbalimbali, lakini pia mpe kipaumbele kwa kila kitu. Hili halihitaji elimu ya darasani. Chunguza wenzako wanaowapa wenzi wao kipaumbele wanavyoishi.
Achana na mifumo ya kizamani, ukimpa mwenzako usawa anajiona ana nafasi kwako na thamani katika uhusiano mlionao.
9. MPE NAFASI
Hapa hakuna kitu kikubwa sana, ni kiasi cha kumpa nafasi katika mambo yako muhimu. Mathalan unataka kununua kiwanja Gongo la Mboto; Hata kama umeshaweka kila kitu sawa, lakini kumshirikisha tu, kutamfanya ajione mwenye nafasi kubwa kwako.
Hili si kwa wanaume pekee, hata wanawake nao wanapaswa kutoa vipaumbele kwa wanaume zao. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa sana kuongeza ladha ya mapenzi kwa wapendanao.
Inawezekana elimu hii imekupitia kushoto, hebu jaribu uone mafanikio yake.
Kumpa nafasi mwenzako katika mambo yako, tafsiri yake ni kumuamini na kumfanya azidi kujiamini kwako. Ni rahisi sana, lakini habari njema kwako ni kwamba, atakusikiliza kwa kila kitu, maana anajiona yeye ni sehemu yako kikamilifu.
10. MTAMBULISHE
Mapenzi ya siri yana ukomo wake marafiki zangu. Ngoja niwaambie, unapokuwa unapenda mapenzi ya siri sana, unampa wakati mgumu mwenzako.
Ni rahisi kufikiria kwamba, unafanya hivyo kwa kuwa ama hujiamini au una mtu mwingine. Weka mambo hadharani. Mtambulishe mwenzi wako kwa marafiki zako.
Jiamini, unapokutana na mtu uliyesoma naye zamani au kuishi naye sehemu moja, mwambie kwamba uliyenaye ni mwenzako na unatarajia kuingia naye kwenye ndoa.
Kufichaficha kunaondoa utamu wa mapenzi. Kunazidisha maswali ambayo hayana majibu. Kama yapo ni huyo mwenzako kujijibu mwenyewe. Kwa kawaida, hatajipa majibu mazuri.
Yatakuwa ya kinyume – yenye tafsiri mbaya. Kwamba yawezekana hutaki kumtambulisha kwa kuwa una mtu mwingine. Je, ni kweli? Kama ndivyo huna sababu ya kumpotezea muda mwenzako. Kama si kweli, basi amka. Gundua kwamba ulikuwa unafanya makosa na uanze ukurasa mpya.
11. GUSIA MAMBO YA KIIMANI
Kuzungumzia mambo ya dini kulingana na imani yenu, kutamsogeza mwenzako kwenye ukweli kuwa una lengo naye la kuungana katika maisha ya ndoa. Angalizo kwako ni kwamba, wakati unamweleza hayo, iwe kweli yanatoka ndani ya moyo wako.
12. WAHUSISHE VIONGOZI WA DINI
Ikiwa uhusiano wenu umekomaa, unatakiwa kuwashirikisha viongozi wa dini. Angalia mazingira, unaweza kwenda naye, au kwenda mwenyewe na kuwaeleza nia yako. Waambie wakuombee au wawaombee ili uhusiano wenu uwe na nguvu.
Kumbuka ndoa ni tendo la heri, hivyo shetani naye hutumia nafasi hiyo kuwaharibia! Kumuingiza Mungu katika uhusiano wenu kuna maana, mtakuwa katika ulinzi wenye nguvu zaidi.
Yamkini pia, kama uliyenaye si chaguo kutoka kwa Muumba atamuengua mikononi mwako na kukupeleka palipo sahihi. Usiogope, nenda kaonane na viongozi wa dini na uwaeleze kinagaubaga.
13. KAMILISHA TARATIBU ZA KIFAMILIA/KIMILA
Ikiwa una uhakika kuwa mwenzako ndiye uliyemkusudia (zaidi kwa wanaume) wajulishe wazazi wako, kisha anza taratibu za kimila na kifamilia. Tuma wazee wapeleke posa, lipa mahari, halafu sasa anza kutimiza maagizo mengine yote utakayoagizwa.
Ni njia ya kuelekea kwenye ndoa. Uhusiano wenye baraka za wazazi, si tu kwamba unakuwa na nguvu, bali una radhi za wazazi wenu wa pande zote mbili. Je, kwa hali hiyo uhusiano wenu hautaimarika? Bila shaka utazidi kuchanua.
Natamani sana kuendelea na vipengele vingine, lakini nafasi yangu hairuhusu, wiki ijayo tutaendelea, USIKOSE!
Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia magazeti ya Global Publishers, ameandika vitabu vya True Love na Let’s Talk About Love vilivyopo mitaani.
3 comments:
No 10 imekaa vizuri sana, ni wengi sana wapo hivyo, ambapo ni makosa makosa makubwa sana.
umri wangu ni miaka 25,natafuta rafiki wa kike baadae awe mke wangu,umri kuanzia miaka 20 -24,,Nafanya kazi serikalini,naishi dar es salaam.nicheki kwa number hii.0755454320 au 0715242345
Post a Comment