ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 10, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. GHARIB BILAL AONGOZA KUAGA MWILI WA STEVEN KANUMBA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Gharib Bilal akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Steven Kanumba ulioagwa leo kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam huku viongozi mbalimbali wa Serikali, viongozi wa dini, Wanasiasa, Wanamuziki Waigizaji na watu maarufu wamejitokeza kuuaga mwili wa mwigizaji huo aliyekuwa maarufu zaidi nchini Tanzania na nje ya  nchi pia, Marehemu Steven Kanumba anazikwa mchana huu kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaamFullshangwe.blog.com inamuvuzisha matukio haya kutoka mjini Dodoma kupitia Sitlite zake zilizotegwa katika viwanja vya Leaders na Makaburi ya Kinondoni kwa matukio zaidi anedelea kufuatilia mtandao wako wa Umma kuhusu tukio hilo kubwa la kihistoria  na la kushtua nchini mwetu kwa kumpoteza mwanafilamu mahiri Steven Kanumba ama Ancle JJ kama alivyojulikana katika moja ya filamu aliyoigiza na watoto na Patcho Mwamba mwanamuziki wa bendi ya  FM Academia
Picha ya chini wa pili kutoka kushoto  ni Mama wa Marehemu Steven Kanumba Bi. Flora Mgoa akiwa katika hali ya majonzi mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akimfariji Mama Kanumba



Mmoja wa waombolezaji akisidiwa na wafanyakazi wa msalaba mwekundu mara baada ya kuzimia katika msiba huo mkubwa.
Kutoka kulia ni Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi, Ridhiwan Kikwete, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Idd Azzan na waombolezaji wengine wakiwa katika msiba huo.
Kundi maalum lililoandaliwa kwa nyimbo za maombolezo likiimba nyimbo za maombolezo katika katika msiba huo.
Jeneza la mwili wa marehemu Kanumba likiwa limewekwa tayari kwa waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho
Ndugu  wa karibu wakielekea sehemu waliyotengewa kukaa.
Askari wa kike wakiweka sawa utaratibu wa waombolezaji kupita katika eneo hilo ili kukaa.
Rais wa Shirikisho la wasanii wa Filamu Saimon Mwakifwamba akizungumza katika msiba huo kutoa salamu zao za rambirambi kwa marehemu Steven Kanumba

Mmoja wa waombolezaji akipitishwa juu juu kwenye vichwa vya waombolezaji ili kupata huduma ya kwanza baada ya kuzirai, katikati anayetazama mbele ni Mussa Kisoky Mkurugenzi wa kampuni ya Sofia Production ya jijini Dar es salaam.
kwa picha na maelezo Bofya Read More
Mwigizaji Steven Jacob kushoto akizungumza  jambo na mbunge wa Maswa Mashariki Mh. John Shibuda katikati.

Mr Mtitu kulia akijadili jambo na mmoja wa waombolezaji wa
Utaratibu unapangwa na wanakamati wa kamati ya mazishi
Gari lililobeba mwili wa marehemu Kanumba linaondoka Leaders kwenda Makaburi ya Kinondoni huku likiwa limezungukwa na waombolezaji.


Umati wa waombolezaji ukiondoka kuelekea makaburi ya Kinondoni.

Jeneza lenye Mwili wa Marehemu,Steven Kanumba likiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam asubuhi hii.  Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Steven Kanumba asubuhi hii kwenye viwanja vya Leaders Club,Jijini Dar es Salaam.akifuatiwa na Mkewe,Pamoja na Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete (mwenye nguo nyeupe kulia). Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu akitoa heshima za mwisho.
Kwaya maalum ikiimba nyimbo za maombolezao katika msimba huo kwenye viwanja vya Leaders
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akipiga sal;ute mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Steven Kanumba kama ishara ya kumkubali kwake na kutoa heshima kwa marehemu Steven Kanumba.

Picha na habari kwa hisani ya FULL SHANGWE

2 comments:

Anonymous said...

yaani nitammisije huyu kaka! RIP Kanumba

Anonymous said...

Bwana ametoa na bwana ametwaa