Advertisements

Friday, April 27, 2012

Rais Sarkorzy ashindwa duru ya kwanza ya uchaguzi

Rais Sarkorzy 
PARIS,Ufaransa

MGOMBEA wa urais kwa tiketi ya chama cha Kisoshalisti nchini Ufaransa,Bw. Francois Hollande, ameshinda duru ya kwanza ya uchaguzi nchini humo.

Huku idadi ya kura nyingi zikiwa zimehesabiwa Bw Hollande tayari amepata asilimia 28 ya kura akifuatiwa na Rais wa nchi hiyo, Bw. Nicolas Sarkozy anafuatia kwa a
silimia 27 hii ikiwa ni idadi ndogo zaidi kwa rais yoyote wa taifa hilo ambaye amewahi kugombea tena kiti hicho.


Haijawahi kutokea kuwa rais  ambaye yupo  madarakani anashindwa kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi.

Na matokeo haya yanampa mpinzani wa Rais Sarkorzy,Bw. Hollande nafasi nzuri sana katika duru ya pili ya uchaguzi huo utakaofanyika baada ya wiki mbili.

Hata hivyo kilicho washangaza wengi baada ya matokeo hayo kutangazwa ni idadi ya kura chama kinacho egemea upande wa kulia kilipata.

Kwa makadirio tu, mtu mmoja kati ya wapiga kura watano nchini Ufaransa alikipigia kura chama hicho, hii ikiwa idadi kubwa zaidi ya kura chama hicho cha Front Nationale kilichopata kwenye uchaguzi wowote nchini humo.

Rais Sarkorzy anasema matokeo hayo yanaonyesha hali ya wasi wasi raia wa nchi hiyo wanayo na ni kura ya maoni dhidi ya utawala wake.

Hata hivyo ametoa changamoto kwa mpinzani wake ajitokeze kwenye mdahalo kati yao kabla duru ya pili ya uchaguzi huo.

Hata hivyo  kutokana na uchache wa kura alizopata dhidi ya Rais Sarkorzy, kiongozi huyo wa chama cha kisoshalisti, Bw.Hollande atakuwa makini sana asipoteze kura muhimu.

Bw Hollande anasema wafaransa wanaimani na mradi wake kwa nchi hiyo ambao umelenga kurejesha haki, usimamizi bora wa uchumi wa nchi, ukuzaji wa nafasi za kazi, kulinda viwanda na kujiandaa vyema kwa siku za usoni.(BBC)

No comments: