Loveness Edwin Mamuya
Kwanza napenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani kwa Watanzania wote wa DMV kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huu wa uchaguzi kufika kwenu kwa wingi ndio kumefanya uchaguzi huu uwe wa kihistoria.
Pia napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote walioniunga mkono katika sera yangu ya MTANZANIA DMV BADILIKA ni jambo lakutia moyo kwa wanaDMV kusema kweli nimeguswa sana na moyo wenu wa upendo mliouonyesha kwangu, hasa timu yangu ya kampeni imefanya kazi ya ziada bila kujali muda wao.
Tatu nampongeza Iddi Seif Sandaly kwa kuchaguliwa dhidi yangu kuwa Rais wetu mpya wa Jumuiya yetu ya DMV popote pale panapo tokea mafahari wawili wanashindana lazima atokee mshindi na mshindwa kwa maana hiyo basi Ushindi wako Iddi Sandaly nimeupokea kwa mikono miwili na daima nitashiriana na wewe katika kusukuma gurudumu la maendelea DMV kama mwanajumuiya mwingine.
Mwisho, nakutakia kila la heri katika kazi yako mpya na naomba Watanzania wenzangu DMV tumuunge mkono Iddi Sandaly na uongozi wake ilikufanya kazi yao iwe rahisi. Asante na Mungu awabariki. MTANZANIA DMV BADILIKA.
5 comments:
nakupenda dada kura nilikupa inaniuma ulivyokosa sisi dmv tunasikitika natamani hata turidie uchaguzi maana hatukutendewa khaki kabisa watu miambili hawakupiga kula?ni kwa nini ?katiba hatujasomewa tumepelekwa mputa sana sana kwanini hawakuchukuwa hata park dmv wamekosa mtu ambaye angeunganisha mimi hamtaniona tena .nilikuja kwa sababu yako wasahau hata fee yangu
Hongera sana Bi. Loveness kwa kuonyesha ukomavu na uelewa pamoja hekima, uungwana na upendo (kama jina lako linavyojieleza:-). Binafsi nimeguswa sana na ujasiri na ungwana wako. Pia wapuuze wote wanaokutupia maneno yasiyokuwa ya ki-ungwana.
Uchaguzi si habari ya Mshinda na Mshindwa. Kilichotokea ni kuwa kura zako hazikutosha tu , BASI:-). Kama kuna aleyeshinda basi ni 'Jumuiya' kwani hatimaye sasa imepata uongozi, kitu ambacho ilikuwa inahitaji kwa muda mrefu.
Hivyo basi ni matumaini yangu kuwa wale hata waliochaguliwa kwenye uongozi hawatalewa kiburi na kutembea mabega juu, bali watakuwa watu kujishusha na kushishirikiana na wale wenzao wenye mawazo na sera mbadala. Congrats and keep up such a good spirit.
HONGERA SANA IDD MWENYEKITI WETU MPYA WA DMV -YES WE CAN
Napenda kutoa shrukrani kwa wana DMV walijitokeza kupiga kura.pili napenda kumpongeza sana Dada yetu Loverness kwa kuonyesha Ukomavu na busara ya hali ya juu kwa kukubaliana na matokeo,na mimi binafsi nakuunga mkono dada loveness,Napia hii itakuwa changamoto kwa wakina mama na dada wote DMV inabidi muuige mfano wa Loveness,PIA wana DMV tubadilike ili ni kwa wote,kutokana na statistics inaonyesha kwamba watu zaidi ya 500 walijitokeza kupiga kura,mfano tukiangalia kinyanganyiro cha mwenyekiti statistics zinaonyesha kwamba,
Idd sandarly alipata kura 205 ambayo hii ni sawa na asilimia 205/500*100=41%
Da loveness alipata kura 119 ambazo hii ni sawa na asilimia 119/500*100=23.8%
kura zilizoaribika ni almost asilimia 35.2%
Back to the point ,kutokana na twakimu izo hapo juu inaonyesha baadhi ya wana DMV bado hatujambua umuhimu wa kupiga kura na kukaa kupiga domo na vijembe kwamba Loveness hafai na Idd , alafu ndo nyienyie ambao mlioaribu kura baadhi yenu kudiriki kuandika ata matusina na ndiyo wa kwanza
mtakao kuwa mnalalamika baada ya miezi kadhaa Uongozi mpya kuingia madarakani, kwamba viongozi mliowachagua awafahi,wana DMV sidhani ktka hiyo asilimia 35% kura zilizoaribika ni zilipigwa na watoto,ukweli ni kwamba baadhi yenu ambao mriharibu kura ni watu wenye heshima na mnaeshimika ktk jumuiya ya DMV.mwana DMV uliyeshidwa kutambua umuhimu wa kura yako tunakuomba ubadilike la sivyo utakuwa aufiti katika jamii.
Mwisho kabisa natanguliza shukrani zangu kwa wana DMV watambua umuhimu wa kupiga kura. na pia wewe Luka aka MPwa naomba nikupe shukrani zangu kwa kuweza kutupa yanayojiri DMV kwa kupita blog yetu ya vijimambo.
MDAU-BLACK MPINGO.
Hongera Idd lakini dada Loveness uko juuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!kama kishada!.Huyu ni Iron Lady wa DMV!mtake msitakeeeeeee!.
Post a Comment