ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 13, 2012

TANGAZO MAALUMU LA MKUTANO WA JUMUIYA YA WATANZANIA DMV TAREHE APRIL/15/2012

TAFADHALI ZINGATIA MUDA UKUMBI UMELIPIWA SAA 3 TU 
2:00 pm -5:00 pm
Ndugu Wanajumuiya,
Kama tulivyowafahamisha hapo awali kuwa kazi mliyotutuma imekamilishwa. Tuna washukuruni wote mlioleta na kutuma mapendekezo yenu kutokea mwanzo mpaka mwisho wa ukamilishaji wa Katiba mpya. Maoni yenu yote yalipokelewa na kufanyiwa kazi ndani ya Katiba, tunashukuru sana kwa mchango na muda wenu mliojitolea kwa nia ya kujenga Jumuiya yetu ya Watanzania DMV.
Hivyo basi, imetufikisha katika hatua kubwa naya mwisho ya kuindeleza mbele Jumuiya yetu. Na kama tunavyojua kuwa kwa sasa hivi hatuna Jumuiya na kamati iliyofanyia marekebisho katiba haina Fedha, Kutokana na hali hiyo, Wanakamati tumependekeza  kama ifuatavyo
-          Tutakuwa na Mkutano mkuu mmoja ambao utashughulikia maswala makuu mawili:

1.      Shughuli ya kwanza itakuwa ya kupitia na kupitisha Katiba.

2.      Shughuli ya pili itakuwa ya uchaguzi mkuu, tutachagua viongozi wa Jumuiya.

Mkutano Mkuu utafanyika tarehe  04/15/2012  saa 8 mchana ( 2:00pm).  Katika
Ukumbi wa  
MIRAGE HALL
1401 UNIVERSITY BLVD
HYATTSVILLE, MD 20783

6 comments:

Anonymous said...

Hapo ndiyo gemu limeanza. Watanzania wanatarajia nini kutoka katika Jumuiya yao? Hapo ndiyo utaona nani anayo mikakati bora ya kusimama na Watanzania. Ubabaishaji hakuna. Kwa interview hii, mimi nimeshapata katibu wangu tayari. Nadhani : Kinyemi 38%, Cherehani 62%

Anonymous said...

Hapa siyo mahali pa kuweka matokeo yako ,wewe uelewi nini madebe wenzako wapigia huko siyo humu.ukweli wote kesho,tumeambiwa tujilekebishe ndiyo maana tumeambiwa watanzani kujirekebisha watu tupo U.S.A lakini akili Zipo Tanzania

Anonymous said...

Hakikisha kuwa unakuja na kitambulisho chako siku ya kupiga kura kuonesha unaishi DMV. Kama huna kitambulisho cha DMV, njoo na Passport yako pamoja na bill inayoonesha kuwa unaishi DMV. Tutalinganisha jina lako kwenye Passport pamoja na anwani iliyoko kwenye Bill ili uweze kupiga kura. Vinginevyo hutaruhusiwa kumpigia kura kiongozi umpendaye.

Anonymous said...

kiongonzi atapatikana tu,hakuna cha usomi wala nini?kama niaka ya nyuma mliongonzwa na hao ambao hawakuwa na usomi wowote na bado waliwaongoza,unaongozwa na watu ambao hata kusafiri nje ya state shida kutoka nchi ndiyo kabisa makaratasi hawana ndiyo viongonzi wa jumuiya,ukitaka kuona balaa waambie kila mtu aje na id yake na police watakuwa pale kuangalia kama utaona mtu tena hao ndiyo wachongaji,ule mkutano wa barozi wenyewe ulikuwa tabu kujiandikisha jamani poleni DC

Anonymous said...

Kwakweli huu ni upuuzi sana!kwanza huyo cherehani HATUJAWAHI KUMUONA POPOTE PALEEEEEEEE!labda hao watu wa kanisani kwake na hapo mnaona kabisa ni kanisani jamnai!yaleyale ya idi ya tamco!sasa hata kama mtu ana PHD haina maana!anaweza kupasi darasani lakini kwenye jumuiya zero!hao watu hawawezi jamani mbona hamuelewiiii????kinyemi kavolunia na utamuona sehemu kibao!!huyo cherehani wapiiiii jamani!?kama msomi ni yeye na familia yake kitabu chake hakiongozi jumuiya ya wabongo!akili zake za darasani sio za kuongoza jumuiya jamaaaa!unaweza kuta mtu ana PHD lakini hawezi kuongoza chochote watanzania wenzangu!tusije kujuta tuliangalie swala hili kiumakini na uangalifu sana!!.

Anonymous said...

Acha kujifanya wewe wa saa 10:17am, ungefika hapo ulipo kama si kwa kutokea tanzania? Kisa USA! Mngekuwa na akili mngebeba box? Sana sana wasomi wakuwahesabu. Chagueni viongozi wenu sio kuisema vibaya Tanzania.