Pia ametumia fursa hiyo kuialika jamii nzima ya Watanzania na wageni waliopo hapa nchini kuhudhuria mkusanyiko utakaofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tarehe 7 mwezi huu wenye lengo la kuzungumzia sababu zilizopelekea kutokea mauaji hayo ya Kimbari, madhara yake, na nini kifanyike ili kuhakikisha matukio kama hayo yahatokei tena si tu Rwanda bali katika Mataifa yote Afrika na Duniani kwa Ujumla. Katika siku hiyo kutakuwa na mashairi, ngonjera, filamu fupi na ushuhuda kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wahanga na walioshuhudia mauaji hayo.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni "Let’s learn from our history to shape a bright future".
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Stella Vuzo akizungumzia maadhimisho hayo yatakayofanyika tarehe 7 mwezi huu ambapo amesema vyombo vya habari ni sekta muhimu ambayo inapaswa kuhudhuria pamoja na jamii nzima kutazama filamu fupi ya dakika 7 inayoonyesha kilichotokea wakati wa mauaji ya kimbari. Kulia ni Afisa kutoka Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama na Kushoto ni Balozi Mdogo wa Rwanda, Mh. Sano Lambert.
Amesema katika maadhimisho hayo watakuwepo viongozi wakaoiwakilisha Serikali ya Rwanda na pia kuhudhuriwa na Msemaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbaria ya Rwanda Profesa Chriss Maina ambapo pamoja na mambo mengine pia atazungumzia maendeleo ya Mahakama hiyo ya Kimataifa ya ICTR.
(Picha kwa hisani ya MO Blog)
No comments:
Post a Comment