ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 16, 2012

ULIKUWA UCHAGUZI WA KIHISTORIA, HAKI NA AMANI

Iddi Seif Sandaly ndio Rais mpya aliyechaguliwa kwenye mkutano wa uchaguzi wa Watanzania DMV uliofanyika katika ukumbi wa Mirage, Iddi Seif Sandaly alishinda kwa kura 205
 
Loveness Edwin Mamuya ambae alikua mgombea wa Urais kwenye mkutano wa uchaguzi uliofanyika Jumapili Aprill 15, 2012 na kupata kura 119.
 
 Jacop Kinyemi aliyekuwa kwenye kinyang'anyiro cha ukatibu mkuu na kuwa  wa pili kwa kura 82, Amos Cherehani ndiye aliyeshinda Ukatibu Mkuu kwa kura 192 na Rhoda Kasamba kwenye nafasi ya ukatibu mkuu alipata kura 40

Wajumbe wa bodi ambao wote walipita kwenye uchaguzi huu kutoka kushoto ni Al- Amini Chande, Dr. Hamza Mwamoyo, Eliserena Kimolo, Grace Sebo Mgaza na Haruni Ulotu.
Maafisa Ubalozi wakifuatilia uchaguzi.
 Mgombea Uraisi Loveness Mamuya (kati) akifuatilia mkutano wa uchaguzi
 Mselem (kushoto) na Dr. Mwamoyo Hamza, Kamati ya kurekebisha katiba ambayo pia ilisimamia uchaguzi wakitayarisha vitendea kazi na kuweka mabo sawa kabla ya upigaji kura
 Mgombea wa Urais Iddi Sandaly (kati) akifuatilia mkutano wa uchaguzi
 Watanzania wa DMV wakiwa mkutanoni
 Watanzania wa DMV ambao Jumapili April 15, 2012 walifika kwa wingi na kuandika historia mpya kwa kuwachagua viongozi watakaoongoza Jumuiya DMV ambayo ilikua inalegalega tangia 2007.
 Umati unakadiriwa kufikia zaid ya 500 wakifuatilia mkutano.
 Wanajumuiya DMV wakimsikiliza Mwenyekiti wa kurekebisha katika (hayupo pichani) alipokua akieleza jambo.

Kwa picha zaidi Bofya Read More


19 comments:

Anonymous said...

Uchaguzi wa kihistoria kweli Mbona haujatueleza Iddy kapata Kura ngapi?

Anonymous said...

ama kweli watu wa DMV mmeamua!

Anonymous said...

ungesoma posts za nyumba ungeona kapata ngapi?

sasa vidole navyo kupiga kura labda mtakuwa mmefukuzisha wale wasio na makaratasi na wenye kuogopa.

sio vizuri msirudie tena

Anonymous said...

Huu kweli ni uchaguzi wa kihistoria!mimi na baadhi ya watu wanaamini Iddi amepata ushindi kwasababu ya Lovenesss,Iddy angekua anagombea na mwanaume mwenzake asingepata kabisaaaa.Ila nampongeza sana Dada Loveness!huyu mwanamke ni shupavu!mjasiri na mtendaji kazi hata kama hana Masters wala PHD lakini ana kisomo cha kuongoza.Hongera sana Loveness.

Anonymous said...

Aibu yenu mliokua mnaandika matusi na dharau na kejeli!hamjui ukweli wa mambo yote!huo ni ushabiki na kuharibiana majina na utu na hamna mlichobomoa ndio kwanza mmejenga,kwani yeyec hajui kutukana hana komputa au yote mliyofanya akarudisha kwenu!!!ni ustaarabu na akili,nampa pongezi sana Loveness umejifungulia njia katika safari yako ndefu ya kugombea chochote hapa usa na afrika,kwanza ni kazi ya hiari wala hulipwi.

Anonymous said...

hivi wewe anony hapo juu unajua unachokiongea ama?acha kuongea pumba.wamemuaribia ama alijiharibia mwenyewe .ustaarabu ni kitu cha bure

Anonymous said...

naomba mnielimishe wapendwa DMV ndio nini?

Anonymous said...

naomba watu mlitambue kwamba japo kuwa dada yetu Loveness kushidwa kwenye uchaguzi huu..lakini atabaki kuwa ni mwanamke ambaye ni shupavu katika jumuiya ya wana DMV.Wana DMV mjivunie kuwa na dada jasiri kama Loveness na sio kukaa na kuanza kumsanifu.je mgegombe nyie mgeshinda?Da loveness na kutakia kila raheri na uendelee na moyo huohuo wa kujitolea katika jamii ya DMV .

Anonymous said...

Wewe Anonymous Apr 16, 2012 08:50 AM; Kwani wewe si mwanaume? Mbona ukusimama na Iddi Ukaona. Wacha Hizo.

Anonymous said...

DC, Maryland, Virginia. (DMV)

Anonymous said...

Watz mbona mnapenda majungu? Kama kura zimepigwa kidemokrasia blahblah za nini?kubali matokeo songa mbele kujenga jumuiya, jukumu la kila mtz. Rais ni moja,aliyeshindwa akae sideline kuchangia mawazo. Wote siwajui bali naboreka na mawazo finyu. Kampeni imeisha,tuwe kitu kimoja sasa kufikia malengo.

Anonymous said...

Loveness ni shupavu hasa, nampongeza kwa kujitokeza ,na pia alipata kura nyingi tu. bado tunakuhitaji DMV ,endelea na kujitolea kwako na mipango yote uliokua nayo ,na wala usirudi nyuma kwa kuwa hukuchaguliwa.
Pia watu wa DMV tuachane na mambo ya udini, ukabila na ubaguzi. Maana kuna jambo nimeliona ila nitanyamaza tu kwa leo. Kila la kheri Iddi. una kazi kubwa ya kuiendeleza jumuiya.
bi mkora DC

Anonymous said...

Uchaguzi umeisha, lets all move on in peace...kuna watu huko FB acheni matusi, u sound pathetic!

Anonymous said...

Ndio maana ukaitwa uchaguzi. Alikuwa anahitajika mshindi mmoja. Kaka Iddi hongera sana. Pia angalia una kazi kubwa ya kuongoza hawa watu. Jitayarishe ndugu yangu, sio kazi ndogo. Nakutakia afya njema, hekima na busara ndio kitu tu ambacho nakuombea kwa Mwenyezi Mungu.

Anonymous said...

Anoyn wa march 16 @o5.35pm,unavyosema ni kweli kabisa,hapa kuna udini,ukabila,tabia mbaya sana ya ubaguzi,niliona kwenye kipindi cha nyuma kuna kaka ambaye simkumbuki jina lake,kasimamia harusi watu wanaanza kujadili kabila yake,na kwanini kasimamia hiyo harusi na wakati wenye harusi wameweka watu wa kabiloa lao tu sasa huo si ubaguzi!leo hii kwenye uchaguzxi tena imezuka dini?kweli tutafika?tujipange.Na wewe hapo juu fikiria sana Loveness hajajiharibia chochote,wewe ni msafi hapo ulipo??jitokeze tukuchambue.

Anonymous said...

Edit profile



Edit profile
OpenID URL:


Edit profile
Name:

URL:


Preview
Edit Anonymous said... ni kweli kuna mtu huko FB ana-act kama mtoto wakati ni mtu mzima karibu anapata na wajukuu. Huyo mtu hata kizungu chake ni vigumu sana kukielewa yet anataka kuleta majungu yasiyo na kichwa wala miguu. kama ni kweli uliyajua mabaya ya mgombea siku nyingi kwa nini usilete malalmiko yako siku zote hizo au kwa nini hukwenda police. tukiamua kuayaweka ya kwake hadharani sidhani kama atahimili. LETS ALL ACT LIKE GROWN UPS PLEASE

Anonymous said...

Anoyn wa hapo juu nakuunga mkono sana,kweli unavyosema,kwanini hakwenda polisi kama ni kweli hakutendewa haki?au akaita watu wenye akili zao kama mashuhuda?na inaelekea alikua anapenda na anafurahia kila moment!1utaona kutokana na kauli zake,kama alikua anakerwa asingekubali,ni makubaliano yao lakini roho inamuuma katupwa.Tena sio kizungu hta kiswahili kuandika hajui kabisaa!ukimya ndio jibu na watu wengi nimeona wanashabikia vitu wasivyovijua kabisaaaa mnasikiliza upande mmoja hamjui mwingine,yaacheni kama yalivyo watu wana chuki zao binafsi nyinyi mnaingilia ugonvi.

Anonymous said...

ni kweli udini umechangia somehow, mie nitaendelea kuwa silent member. Loveness baadaye utakuja kufurahi kwamba hukushinda maana kuwaongoza watu wa DMV yataka moyo na maini!

Anonymous said...

dada loveness unavyokaa kimya na wengine wana tukana ndio unazidi kuonekana your super smart waache wehu waongee wewe focus dada yangu your very smart woman nakuomba sana kaa kimya hata wasema umeouwa wewe kaa kimya