Nape Nnauye akishuka kwenye Ndege alipoanza ziara ya Mkoa wa Kagera
. Asema hata walioanzisha upinzani walitoka CCM, lakini Chama bado ni imara.. Wanaotangazwa kuhamia Chadema siku hizi ni CCM bandiaNA MWANDISHI WETU, BUKOBAKATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema wanachama kuhamia Chadema hakutaiua CCM, kwa kuwa hata walioanzisha vyama vya upinzani na wanachama wao walitoka CCM zaidi ya miaka 20 iliyopita, na hadi leo bado ni imara.Amesema licha kutokuwa tishio kwa uhai wa CCM, wanaotangazwa kuhamia Chadema wengi wao ni bandia, si wanachama halisi wa CCM, isipokuwa chama hicho kimekuwa kikitangaza kupata wanachama wapya kutoka CCM kwa kuwa ni moja ya propaganda waliyobuni kujaribu kuwanyong'onyesha wana CCM, wadhani chama chao sasa kinakufa kwa kuhamwa.Akihutubia kwenye Baraza la mwaka la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), wilaya ya Missenyi mkoani Kagera,Nape aliwataka wanachama wa CCM, kutonyongonyeshwa na propaganda za Chadema au chama chochote cha upinzani kwa kuwa bado ni wengi, na Chama Cha Mapinduzi kipo katika mikono imara na salama.Nape alisema, katika propaganda hizo, Chadema wamekuwa wakiwakusanya kutoka maeneo mbalimbali wafuasi wao na kuwapeleka kwenye mikutano yao na kuwatangaza kuwa ni wana-CCM wanaohamia kwao.Alisema mbali na hivyo Chadema huwatafutia sare na kadi za CCM wafuasi hao ili wanapotangaza kujiunga na chama chao, wasiohiji au kuona mbali waamini kwamba wanaohusika kwenye kuhama huko ni wanachama hasa wa Chama Cha Mapinduzi.Nape alisema, propaganda kama hiyo na nyingine ambazo wamekuwa wakizusha Chadema kwa kutanagaza uongo, ni mpango wa kujaribu kuiondoa CCM kwenye lengo lake la kuwatumikia wananchi kama chama tawala, kwa kuwa Chadema kinajua kikifanikiwa wananchi wataichukia sana CCM kwa serikali yake kutowatekelezea ahadi ilizowapa kwenye ilani ya uchaguzi."Chadema tumeshawastukia, wameshaona kwamba kwa sera hawatuwezi, sasa wanajaribu kutuondoa kwenye reli, tuache kushughulika na utekelezaji wa ilani yetu ya uchaguzi kuwahudumia wananchi. Sisi tutaendelea kuwapuuza na ninyi wana-CCM wapuuzeni, maana wakati tutakapokuja kuwaomba tena kura wananchi watatuuliza tulichowafanyia, hawatatuuliza tumewajibu nini Chedema", alisema Nape.Alisema, si kweli kwamba CCM haioni matatizo yanayowakabili wananchi ikiwemo kupanda kwa gharama ya maisha, inaona na ndiyo sababu Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyokutana mapema mwezi huu mjini Dodoma, pamoja na mambo mengine iliitaka serikali kutafuta njia zitakazoweza kupinguza hali hiyo.Nape aliwataka wanachama wa CCM na hasa vijana, kutumia uchaguzi wa CCM katika ngazi mbalimbali kuchagua viongozi imara na safi katika jamii, ili katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 CCM iingine ikiwa na viongozi bora wanaoweza kutetea maslahi ya wananchi kwa dhati.Aliwataka wana-CCM kuepuka kupewa rushwa na wagombea wanaotaka kupata nafasi kupitia njia haramu kwa sababu wanaojaribu kutumia rushwa katika kutafuta uongozi hawajiamini usafi wao.Kuhusu wana-CCM wanaotishia kuhamia upinzani kwa kunyimwa uongozi ndani ya CCM kupitia njia halali, Nape aliwataka wana-CCM kuwa tayari kuwaacha viongozi hao wahame, akisema, kwa kuwa anayetishia kuhama CCM huyo amekwisha hama kiroho ila mwili wake ndio umebaki CCM.Mapema Katibu wa CCM, wilaya ya Missenyi, Philibert Ngemela alisema, katika baraza hilo jumla ya wajumbe 500 wamekutana kutoka katika kata 14 za wilaya hiyo kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ikiwemo uhai wa jumuia hiyo na CCM.
No comments:
Post a Comment