ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, May 5, 2012

NGORONGORO HEROERS YASONGA MBELE KWA GOLI LA UGENINI


Timu ya taifa ya U20 Ngorongoro Heroers imefanikiwa kuitoa nje ya mashindano timu ya  Sudan mjini Kahartoum usiku huu baada ya kufungwa magoli 2-1 na wasudan hao,  ikisonga mbele kwa goli la ugenini, kwa matokeo hayo ina maana timu ya Ngorongoro Heroers imesonga mbele kwa magoli 4-3 dhidi ya timu ya Sidan.


Goli la timu ya Ngorongoro Heroers limefungwa na mshambuliaji wa timu ya TP Mazembe Thomas Ulimwengu katika dakika ya 12 ya mchezo, wakati magoli ya timu ya Sudan yakifungwa na Mohd Abdelrahman dakika ya 10 na goli la pili likifungwa kwa penati na mchezaji Ahmed Nasr dakika ya 65 ya mchezo, hongereni sana vijana mmefanya kazi nzuri.

Picha na Habari kwa hisani ya FULL SHANGWE

No comments: