Jeshi la Polisi hapa nchini limetajwa kuwa taasisi ya serikali inayoongoza kwa kupokea rushwa huku Tanzania ikishika nafasi ya tatu kwa vitendo hivyo katika nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), mwaka 2011.
Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya haki za binadamu iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kwa mwaka 2011.
Ripoti hiyo ilizinduliwa jana jijini Dar es Salam na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Polisi wanaoongoza kwa rushwa kwa asilimia 36.2, wakifuatiwa Mahakama asilimia 32.4, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), asilimia 15.1, Hospitali asilimia 8.6, na Wizara ya Ardhi imepewa asilimia 5.3.
Katika ripoti hiyo Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni za (Brela), ndiyo taasisi iliyoonekana kutojihusisha na vitendo vya rushwa ambapo imeshindwa kupewa asilimia yoyote.
Ripoti hiyo ilisema kwamba Tanzania kwa mwaka 2011 ilishika nafasi ya tatu kwa vitendo vya rushwa kwa asilimia 31.6, Uganda asilimia 33.9. Kenya asilimia 28.8, Rwanda asilimia 5.1 huku Burundi ikiongoza kwa kuwa na asilimia 37.9.
Aidha, ripoti hiyo imeeleza kwamba mwaka 2011 jeshi la Polisi liliua raia 25 kwa risasi, huku watu 673 wakiua na wananchi wenye hasira katika matukio mbalimbali.
Mkoa wa Dar es Salaam umetajwa kuwa unaongoza kwa mauaji yanayotokana na watu wenye hasira ambapo ripoti inaonyesha kwamba mwaka 2011 watu 150 waliuwa.
Baadhi ya mikoa na idadi ya watu waliouawa kwenye mabano ni Mbeya (43), Mwanza (84), Shinyanga (80), Kilimanjaro (59), Tabora (58), Kagera (33), Mara (20), Tanga (16) na Morogoro (15).
Ripoti hiyo ilibainisha kwamba mwaka 2011 wanananchi waliwaua polisi watano katika mikoa mbalimbali hapa nchini kuanzia Januari hadi Desemba.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Profesa Lipumba alisema LHRC imekuwa ikiibua vitu vingi ambavyo vinachangia kuibua, kuielimisha, kulinda na kutetea haki za binadamu hapa nchini.
Profesa Lipumba aliwakumbusha viongozi wa nchi kuwa waadilifu na kuachana na vitendo vya ubadhirifu wa fedha za wananchi zinazotokana na kodi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa LHRC, Dk. Hellen Kijo- Bisimba alisema vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu hapa nchini vinaongezeka.
Alitaja baadhi ya vitendo hivyo kuwa ni pamoja na kuendelea kuwepo kwa adhabu ya kifo, unyanyasaji wa majumbani, mauji yanayofanywa na wananchi pamoja na ajali za barabarani.

CHANZO: NIPASHE
1 comment:
Hongera Mh.Lipumba kwa kuzindua hiyo ripoti ya RUSHWA! sasa ni wakati umefika kwa wala RUSHWA wakamatwe na wachukuliwe hatua kali sana ili iwe fundisho kwa wengine,Hata hizo asilimia mlizozitaja ni ndogo sana maana wala Rushwa ni wengi sana kuliko mnavyofikiria!Ni aibu tupu Tanzania ipo katika namba tatu kati ya nchi tano za Afrika wala RUSHWA! Ubinafsi ni mwingi sana na kila mtu anafikiria tumbo lake! Ni bora mtutetee sisi wanyonge tunaodaiwa RUSHWA kwa nguvu,hatupati haki na huduma tunayostahili hadi tutoe RUSHWA!
Post a Comment