NAOMBA KILA MTANZANIA POPOTE ULIPO UFUMBE MACHO KWA DAKITA MBILI TU KISHA JIULIZE;
- Kwa nini mimi ni Mtanzania?
- Isingekuwapo Tanzania ningekuwa wapi? Kwa watu wengine?
- Kama ninachukua rushwa ni kiasi gani kinatosha? (How much is enough?) ni yadi au mita ngapi maji yanaweza kuruka kuacha nyuma? (How many yards can water skip behind?)
Dakika mbili za kujiuliza zimekwisha, watanzania napenda kuwakumbusha kuwa tuna kazi kubwa sana mbele yetu, kizuri tunaiweza.
- Elimu, tuboreshe elimu yetu hasa kwa vitendo, kama vile ufundi magari, uselemala, nk.
- Teknologia ni muhimu sana. Tuanze kuunda magari yetu wenyewwe, matrekta na mashine ndogondogo za umwagiliaji mashambani. I don’t care where we get that technology just let’s get it. Tukaibe teknologia popote ipatikanapo hata kwa kununua.
Mashambani kutakuwa na ajira (Kilimo) na mijini ajira (viwanda na uzalishaji mwingine). Kutengeneza pesa bila kuzalisha mazao(products) au huduma (services) ni dhambi kubwa sana watanzania tunatakiwa tuondokane nayo.
- Huduma za afya ziboreshwe mahospitalini. Madaktari, manesi na watumishi wote wa huduma za afya waweke moyo wa uduma bora mbele na pesa zitakuja baadaye. Hakuna kitu kizuri kama kuangalia kitu ulichofanya na umekifanya vizuri. Kabla ya watu wengine kusema, wewe mwenyewe unaridhika kuwa nimefanya kazi yangu vizuri.
- Miundombinu; tupanuwe na kuongeza mabarabara mapya katika vijiji, miji na majiji yetu. Msemo wa kusema hatuna pesa tuache nyuma yetu, badala yake tuseme tukamue (squeeze) kila shilingi mpaka kieleweke.
- Nishati; tuwekeze katika nishati zote tulizonazo, umeme wa maji, makaa ya mawe, gesi ya asili, umeme wa jua, ikiwezekana umeme wa nyuklia. Kukiwepo na nishati ya uhakika ni rahisi kuwekeza na kutengeneza ajira za kazi.
- Nyumba na mazingira bora ya kuishi; turekebishe miji yetu iwe ya kisasa kwa kujenga nyumba zetu kwa mpangilio hasa katika majiji yetu. Usafi wa mazingira ni kitu kingine watanzania tunahitaji kuweka kipao mbele. Tusitupe taka ovyo na ikiwezekana tupande nyasi kuzunguka nyumba zetu tupunguze mavumbi. Tukiweza kutokomeza mbu na nzi tutakuwa tumefanya kazi nzuri sana.
- Mwisho kabisa maji safi ya kunywa.
Kila kitu hapo juu kitafikiwa na kufanikishwa siyo kwa miujiza bali tu, ikiwa kila mtanzania atashiriki kikamilifu kwa kufanya kazi kwa bidii, maarifa, kushauri mbinu mbalimbali, kujituma kwa moyo wake wote na kujiuliza swali moja;
“KAMA SIYO MIMI TANZANIA ITAJENGWA NA KUENDELEZWA NA NANI?”
Baba wa yote ni KATIBA yetu na utawala wa sharia. Tushirikiane na tumsaidie Rais wetu, serikali yetu, badala ya kulaumu na kunung’unika, tupige kazi watanzania.
Mungu ibariki Tanzania, mbariki Rais Kikwete na marais wote waliomtangulia, wabariki wabunge wetu wawe na miyoyo ya kuijenga nchi yetu kwa dhati, Mungu wabariki watumishi wa serikali yetu na watanzania wote kila siku tujiulize maswali mawili kabla ya kwenda kulala;
1. “NIMEFANYA NINI LEO CHA KUJIVUNIA CHA KUJENGA NCHI YANGU?”
2. “NIMEFANYA KITU CHOCHOTE KIBAYA CHA KUIHUJUMU NCHI YANGU KAMA VILE RUSHWA, WIZI NK?
Jibu litakupa dira nzuri na kufanya kitu sahihi.
Aksante. Mdau wa Morogoro Mji kasoro bahari.
1 comment:
Haya mawazo yametulia, yamenifanya kutaka kulia.
Nimemkumbuka Mwalimu Nyerere katika moja ya hotuba zake za mwanzo kabisa aliposema
"Namuomba kila Mtanganyika/Mtanzania ale kiapo kuwa atamuangamiza adui umasikini(poverty) kila atakapomuona utajiri wa Tanganyika bado upo aridhini".
Naamini makala hii itachangiwa na wengi kwani inaeleweka.
Post a Comment