ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 11, 2012

Rais Mstaafu Mwinyi awalipua Uamsho


  Ataja pia Boko Haramu, Al Shabab na Al Qaeda
  Maaskofu nao walaani vurugu
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi
Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, amewatahadharisha waumini wa madhehebu ya dini ya Kiislamu nchini kujiepusha na vikundi vya Al Shaabab, Boko Haram, Al-Qaeda na Uamusho kilichopo Zanzibar vinavyotumia mwavuli wa dini kufanya uhalifu na kuvuruga amani nchini.

Alhaji Mwinyi alitoa tahadhari hiyo kwenye ufunguzi wa msikiti wa Muhajirina uliopo  Kata ya Majengo, katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida.

Alisema kwamba katika siku za hivi karibuni kumezuka vikundi vya baadhi ya watu wanaotumia mwavuli wa dini ya Kiislamu kufanya vurugu kwa visingizio vya kudai maslahi ya waumini wa madhehebu ya dini ya Kiislamu.


Kwa mujibu wa Mzee Mwinyi, vikundi hivyo ni vya shari vyenye kujihusisha na vitendo viovu kama vile kuchoma nyumba, makanisa na hata kupiga watu kwa madai kwamba wanapigania Uislamu.

Alisema kuwa kutokana na vitendo hivyo ambavyo ni kinyume cha sheria ambavyo pia havipiganii haki za Uislamu, vimechangia amani, utulivu na usalama kutoweka miongoni mwa jamii.

“Vimezuka vikundi vinavyoingiza vita misikitini, vinaingia na mabomu misikitini na hivyo kusababishia waumini vifo,” alisema na kuongeza: “Na kundi lililoathirika zaidi na vitendo hivyo viovu ni la vijana kwani ndiyo wahusika wakuu na masuala hayo.”

Alhaji Mwinyi alitumia fursa hiyo ya ufunguzi huo wa msikiti kuwaonya waumni hao kutokuwa wafitini, wazabizabina, wasengenyaji na wachukuaji wa maneno kutoka sehemu moja kupeleka sehemu nyingine kusikohusika.

Alisema msikiti alioufungua utakuwa ukitumika kama chuo na utajihusisha zaidi na mambo ya kheri na siyo kuchochea mifarakano miongoni mwa waumini na jamii kwa ujumla.

Kikundi cha Al-Qaeda lilikuwa kiendesha harakati zake katika nchi za Afghanistan na Pakistan, lakini hivi sasa kina matawi katika nchi mbalimbali duniani. Boko Haram kipo nchini Nigeria wakati Al Shaabab Somalia.

MAASKOFU NAO WALAANI VURUGU

Kanisa Katoliki nchini limetoa tamko zito likilaani vurugu na vitendo vya uasi vilivyofanywa na watu wanaodhaniwa kwamba ni wafuasi wa kikundi cha Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (Jumiki), likisema  uasi huo haukubaliki na waliofanya vitendo hivyo wamepotoka.

Vurugu hizo zilizotokea Mei 26, mwaka huu na kudumu kwa siku tatu, zilisababisha hasara kubwa ya mamilioni ya fedha, ikiwemo uchomaji moto nyumba za ibada, uporaji wa mali za raia na wafanyabiashara.

 Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea, Mhashamu Norbert Mtega, alisema kuwa hakuna sheria wala dola yeyote duniani, inayoweza kumzuia mtu kuabudu dini aitakayo na kwamba wanaofikiri wanaweza kufanya hivyo wanakosea.

Askofu Mtega aliyasema hayo wakati akiongoza maelfu ya waumini wa kanisa hilo kutoka mikoa mbalimbali nchini kwenye kilele cha maadhimisho ya 50 ya kimataifa ya kongamano la Ekaristi Takatifu lililofanyika katika Parokia ya Kihesa, Jimbo Katoliki la Iringa.

“Wanaotuzuia tusiabudu ekaristi takatifu wamekosea, maana hakuna sheria wala dola yeyote inayoweza kumzuia mtu asiabudu kwa kuwa kama umeumbwa na Mungu lazima umwabudu Mungu,” alisema Askofu Mtega.

Rais wa TEC, ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Kuu la Mwanza,Yuda Thaddeus Ruwa’ichi, alisema kuwa kutokana na hali iliyojitokeza visiwani Zanzibar, alilazimika kuzungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Zanzibar, Augustino Shao, na kumuomba asihudhurie kongamano hilo ili aendelee kukaa na waumini wake na kuwapa matumaini kwa yaliyojitokeza.

“Hapa hamjamuona Askofu la Zanzibar, Mhashamu Augustino Shao, hii ni kutokana na hali iliyojitokeza kule visiwani Zanzibar.

Nilizungumza naye kwa kirefu nikamwambia asije ni vyema aendelee kushikamana na watu wake katika kipindi hiki kigumu ili awape matumaini…Sisi tuna wazawadia amani,” alisisitiza Rais huyo wa TEC.

MUUNGANO

Kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Askofu Mtega aliwataka Watanzania kutunza tunu hiyo waliyopewa na Mwenyenzi Mungu huku akihoji yalipotokea mawazo potofu ya baadhi ya Watanzania wanaotaka uvunjwe.

“Wanaotaka tubomoe palipo na umoja wetu wana lao, hawataki kutunza tunu waliyopewa na Mwenyenzi Mungu kwa hiyo mimi nafikiri wanaotaka tutengane tuwapige vita na wala tusiwaonee hayo,” alisema na kuhoji: “Hivi haya mawazo ya kuvunja Muungano yanatoka wapi?”

Katika kongamano hilo lililohuduriwa maelfu ya waumini, maaskofu wapatao 21 kutoka mikoa mbalimbali nchini, viongozi wa serikali, vyombo vya dola na viongozi wa vyama vya siasa walishiriki maandamano makubwa kutoka kanisa la Consolatha hadi makao makuu ya Kanisa Katoliki Jimbo la  Iringa, Kihesa.





 
CHANZO: NIPASHE

4 comments:

Anonymous said...

laana ya mungu daima iko kwake alishindwda kukemea kuchomwa kwa quran tukufu kule Arusha na mwanza na nishakushutukia wewe dj luke kazi yako kuweka post za uchochezi tu na kuiponda taasisi ya UAMSHO, MDINI MKUBWA WEWE na comment zinazo data huziweki unaziweka hizi tu zinazokubrudisha roho you are not like michuzi kila comment yeye anaweka hata uki mtusi jirekebishe mkuuu na hii ka blog chako

Anonymous said...

ndo maana alichapwa vibao huyu mwinyi na vitoto vidogo vidogo na akijitia kimbele mbele zaidi atachapwa tena mwili mzima kama mtoto mdogo asubiri arbaini zake

Anonymous said...

Ndugu yangu, if you cannot positively contribute, just keep quiet. No one will accuse you of being quiet.

Anonymous said...

Nimesoma habari zilizoandikwa kuhusu alichosema Mzee Mwinyi, lakini sijaona kitu chochote kinachomfanya astahili lawama zako. Alichofanya Mzee wa watu ni kuhubiri amani, kitu ambacho ni nguzo ya jamii na dini zote.