![]() |
| Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrodi Mkono |
Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrodi Mkono, amesema mbinu chafu zilizofanywa na Wakenya dhidi ya barabara ya Serengeti inayoanzia katika kijiji cha Mukutano kupitia kijiji cha Butiama, kijiji cha Ikizu kwenda kijiji cha Nata, zimeifanya Serikali ya Tanzania kushindwa kuijenga licha ya kupiga kelele kwa zaidi ya miaka 12 iliyopita.
Pia amelaumu upendeleo ambao umekuwa ukifanywa na Serikali kwa kujenga barabara za mikoa mingine, huku ikiisahau barabara, ambayo Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliusia ijengwe.
Mkono, ambaye ni mwanasheria maarufu ndani na nje ya nchi, alisema hayo juzi jioni wakati akichangia mjadala kuhusu Mpango wa Maendeleo na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2012/2013 yaliyowasilisha na Waziri wake, Dk. John Magufuli, bungeni mjini hapa juzi.
Takriban miaka 12 iliyopita amekuwa akipiga makelele bungeni akiulizia hatima ya barabara hiyo, lakini kelele zake zimekuwa zikiishia patupu.
“La ajabu sana ni kwamba, ile barabara tuliyoahidiwa nyuma huku, itapita Serengeti, basi Wakenya wamefanya mbinu chafu kuhakikisha barabara hiyo haijengwi,” alisema Mkono na kuongeza:
“Badala yake, wanaharakisha kwa kasi sana barabara kutoka Sirari kwenda Mwanza. Ndiyo unaona kweli ujenzi unajengwa pale. Lakini barabara ya Bgadimno serikali imenyamaza. Nataka kupata kauli ya serikali, kuhusu hii barabara ya Serengeti, ni nini, ‘tumesarenda’, tumebwaga silaha chini na kusalimu amri kwa watu wa Kenya kwa kutuzuia tusiende Serengeti?”
Pia alisema upande wa Mara, barabara imekuwa haina umuhimu sana kutumika kupeleka mazao wilayani Serengeti.
Alisema hivi sasa barabara hiyo imekatwa, ambapo inatoka kijiji cha Nata na kuishia katika kijiji cha Mukutano bila kujulikana inakopitia.
Zaidi ya hivyo, alisema amebaini kuwapo ujanja unaofanywa na serikali katika ujenzi wa barabara kwa kuwa zipo barabara za mikoa mingine zimejengwa haraka, lakini nyingine zinaishia kuchomekwa.
“Barabara ile ya Kilosa, haiko kwenye Ilani, iliwekwa tu. Kilosa, Dumila, hapo hapo imekwenda, imetengewa fedha inajengwa,” alisema Mkono.
Wakati barabara ya kama ya Kilosa ikipewa upendeleo huo, takriban miaka 40 sasa, barabara ya Nyerere inatengewa Sh. bilioni tatu kwa ajili ya ujenzi.
Kutokana na hali hiyo, aliahidi kutounga mkono bajeti ya wizara hiyo kwa sababu tu ya barabara ya Nyerere kusahauliwa.
Alisema pia Rais Jakaya Kikwete aliwahi kwenda Busekera na kuwaambia wananchi wa huko kuwa wamuachie hiyo barabara hiyo, ambayo alisema imetajwa pia kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba, lazima ingejengwa, lakini hadi sasa haoni chochote kinachofanywa kuhusu barabara hiyo.
“Niwaambiaje wananchi wale? Nikienda kule wananiuliza, Rais aliahidi, mbona chochote hakiendelei? Nataka kujua hawa watu waende wapi? Mazao yao yote ziwani yanaishia pale. Hawaruhusiwi kwenda Serengeti, wayapeleke wapi?” alihoji Mkono na kuongeza:
Alisema pia barabara nyingine ambayo ni muhimu ni ile inayotoka Kirumi kupitia Kiagata mpaka Serengeti, ambapo kila wakati madaraja yamekuwa yakivunjika, lakini haoni serikali ikifanya lolote kuhusu barabara hiyo.

CHANZO: NIPASHE
(1).jpg)
No comments:
Post a Comment