ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 31, 2012

JAJI WARIOBA AWAONYA WANAOWAFUNDISHA WANANCHI JINSI YA KUCHANGIA KATIBA MPYA

MH: TUNDU LISSU AKIPEANA SALAAM NA WAALIKWA 

secretari ya Chama cha wanasheria Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na jaji Warioba ambaye ndie alikuwa mgeni rasmi wa mkutano wa chama cha wanasheria Tanzania
MWENYEKITI wa Tume ya Katiba mpya hapa nchini Jaji Joseph Sinde Warioba amezitaka baadhi ya Taasisi ambazo zinawafundisha wananchi jinsi ya kuchangia maoni katika mchakato wa Katiba Mpya kuacha mara moja na badala yake wananchi wenyewe wachangia mawazo yao kulingana na Uitaji wa Jamii zao
Jaji Warioba aliyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa Nusu mwaka kwa wanachama wa chama cha wanasheria hapa Nchini (Tanganyika Law Society) uliofanyika katika ukumbi wa Simba ulioko ndani ya jengo la mikutano la kimataifa AICC
Aidha Jaji Warioba alisema kuwa kwa sasa wapo baadhi ya watu ambao wanawafundisha wananchi jinsi ya kuchangia mawazo yao kwenye tume hiyo ilihali wananchi hao bado wanakabiliwa na changamoto ambazo ni muhimu sana kuwepo kwenye mchakato huo wa Katiba mpya.
Alifafanua kuwa hali hiyo ni ya ukandamizaji sana kwani wananchi wanakosa Uhuru wao na badala yake wanasema na kujadili kile ambacho baadho ya Taasisi na Mashirika wanachokitaka tofauti na Makusudio ya Tume hiyo
“tunajua kuwa kwa sasa wapo baadhi ya wananchi ambao hawajui na hawatambui kabisa masuala haya ya Katiba kwa kuwa hawana elimu yake lakini bado wana nafasi kubwa sana ya kuweza kuchangia wanachokitaka kiwepo kwenye masuala hayo ya Katiba na sasa hawa watu, Taasisi, na wengineo wasitumie mwanya huo kuwashawishi watu waweze kutoa maoni wanayoyataka wao na kuacha yale ya msingi ambayo yapo ndani ya Jamii zao”aliongeza Jaji Warioba
Pia alisema kuwa nao Wanasheria wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakuwa mabalozi wazuri hasa katika kutangazia Umma umuhimu wa kushirikii na kuchangia Katiba mpya kwani Katiba na Sheria havipangani bali vinaendana kwa pamoja
Awali Raisi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Bw Francis Stolla alisema kuwa ili kukabiliana na masuala mbalimbali ambayo yanajitokeza katika Katiba, wanachama wa chama hicho Watajadili kwa pamoja ambapo mara baada ya majadiliano watatoka na maazimio mbalimbali ambayo yatalenga kujenga na kuimarisha Mchakato mzima wa Katiba mpya
Bw Stolla aliongeza kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa na nafasi kubwa sana ya kuweza kulinda Umma wa Watanzania kutokana na hali hiyo wadau wa Sheria wana nafasi kubwa sana ya kuweza kusaidia Serikali hasa katika zoezi la Ukusanyaji wa Maoni yahususyo Katiba mpya.
“Sheria ya Chama chetu ni kusaidia Serikali juu ya masuala ya Sheria kwa hali hiyo hili pia ni letu na hivyo ni vema basi kama kila mdau ambaye anahusika na Sheria akahakikisha kuwa anatoa elimu zaidi hata kwa wale ambao hawana elimu juu ya umuhimu wa kutoa Maoni ya kuunda Katiba mpya ya Nchi”aliongeza Bw Stolla

No comments: