kamanda wa polisi mkoani Arusha
JAMBAZI sugu lililokuwa likitafutwa kwa muda mrefu mkoani hapa,aliyetambulika kwa jina la Peter Toshi
mkazi wa dareaja mbili jijini ARUSHA, amekufa baada ya kupigwa risasi
na askari polisi katika majibishano ya kurushiana risasi wakati
akijiandaa kufanya uhalifu akiwa amefuatana na mwenzake.
Kamanda
wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo
limetokea agosti 29 mwaka huu majira ya saa 5 usiku katika eneo la
Sinoni daraja mbili ndani ya manispaa ya Arusha.
Sabas
alisema kuwa,kuuawa kwa jambazi huyo ambaye alikuwa akitafutwa muda
mrefu ni baada ya wasamaria wema kutoa taarifa kwa jeshi la polisi
kuhusiana na watu hao ambao ni majambazi baada ya kuwatilia mashaka.
Alisema kuwa jambazi huyo
akiwa na mwenzake walikuwa wamesimama katika eneo la bar ya tanzanite
iliyopo eneo la sinoni ambapo walikuwa wakijiandaa kwa ajili ya kwenda
kufanya uhalifu .
Alisema
kuwa, baada ya polisi kupata taarifa hiyo walifika eneo la tukio,
ambapo majambazi hao walipowaona polisi ghafla walianza kuwarushia risasi ndipo polisi walianza kujibu mapigo na hatimaye kufanikiwa kuumpiga jambazi huyo ambaye alifariki dunia.
Alifafanua
kuwa, katika majibizano hayo ya risasi jambazi mwingine alifanikiwa
kukimbia na jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi katika
kumsaka aliyekimbia.
Aidha baada ya jambazi huyo,kufariki alipekuliwa na kukutwa na silaha moja aina ya Pistol aina ya Tisas ikiwa imefutwa namba zake huku ikiwa na risasi 3 tu.
Alifafanua
zaidi kuwa, jambazi huyo hivi karibuni alitoka mahabusu akikabiliwa na
tuhuma mbalimbali za mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha na amekuwa
akiendelea na uhalifu mkoani hapa na jeshi la polisi limekuwa likimsaka kwa muda mrefu sana.
Sabas
alisema kuwa, jeshi la polisi mkoani hapa linaendelea na uchunguzi
zaidi kuhusiana na tukio hilo, na amewaomba wananchi mbalimbali
kuhakikisha kuwa wanatoa ushirikiano wa kutosha klatikakuwafichua
wahalifu wote.
Hata
hivyo taarifa kutoka eneo la tukio zimedai kuwa jambazi huyo akiwa na
mwenzake alipanga kwenda kufanya mauaji kwa mkazi mmoja wa eneo
hilo(jina limehifadhiwa) anayedaiwa kuwa ni rafiki yao baada ya kubaini kuwa amekuwa akiwasaliti kwa kutoa taarifa zao za uhalifu kwa polisi.
Mwili
wa jambazi hiuyo umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitaloi
ya mkoa mount meru kwa ajili ya uchunguzi huku jeshi hilo likiendesha
msako ka jaambazi mwingine aliyefanikiwa kutoroka.
1 comment:
Huyu alikuwa na tuhuma za mauaji na unyang'anyi wa kutumia nguvu inakuwaje anatolewa jela wakati ni mhalifu?
Post a Comment