ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 29, 2012

TUSKER LAGER YAMWAGA DOLA 450,000 KUDHAMINI KOMBE LA CHALENJI


 Mkurugenzi wa masoko wa EABL kanda ya Uganda, Lemmy Mutahi katikati akikabidhi mfano wa hundi kwa katibu mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye kulia ni makamu wa Raisi wa shirikisho la soka Uganda (FUFA)Livingstone Kyambadde.
 Katibu mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye akipokea kombe litakalokabidhiwa kwa bingwa wa mwaka huu wa michuano ya Chalenji kutoka kwa Mkurugenzi wa masoko wa EABL kanda ya Uganda Lemmy Mutahi  katika hafla iliyodfanyika leo Serena Hotel, Kampala. Kulia ni Makamu wa raids wa  FUFA,Livingtone Kyambadde.
Katibu Mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye akitaniana na mmmoja ya wajumbe waanzilishi wa  Cecafa Kezekia Ssegwanga Musisi kabla ya kuzinduliwa kwa michuano ya Cecafa -Tusker Cup 2012 , serena Hotel Kampala leoo.

KAMPUNI ya East Africa Breweries (EABL) kupitia bia ya  Tusker  Lager imemwaga dola za kimarekani 450,000 kwa ajili ya kudhamini michuano ya Tusker Chalenji itakayofanyika kuanzia Novemba 24 hadi desemba 8 mwaka huu katika viwanja vya Namboole na Mandela Kampala, Uganda.
Hafla ya kusaini mkataba huo imefanyika leo  katika hoteli ya Serena Kampala ambapo Katibu Mkuu wa Baraza la vyma vya soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Nicholaus Musonye alibadilishana hati za mkataba na mkurugenzi wa Masoko wa EABL kanda ya Uganda, Lemmy Mutahi.
Aidha, dola  USD 60.000 zimetengwa kwa washindi ambapo mshindi wa kwanza atapata dola 30.000,mshindi wa pili Dola 20.000  na wa tatu dola 10.000 huku michuano hiyo itarushwa live na kituo cha Televisheni cha Super Sport.
Nchi zitakazoshiriki ni pamoja na Burundi, Djibouti, Ethiopia, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Somalia, South Sudan, Uganda, Tanzania, Sudan na Zanzibar.

Habari na picha na Dina Ismail Blog

No comments: