Marehemu DR. Yussuf Saleh Salim
Bibi Nadra Salim, anatoa shukrani zake za dhati kwa ndugu jamaa na marafiki zake wote waliokuwa nae pamoja katika kipindi chote kigumu cha kuombeleza msiba wa marehemu mume wake mpenzi, mpaka hapo jana alipotoka ndani (kizuka).
Kusema asante haitoshi kwa makubwa mliyoyafanya, mshikamano, umoja, ushirikiano na ukaribu mliompa kwa kipindi hiki chote amefarijika sana, haoni chochote atakachowalipa kitakacholingana na yote hayo zaidi ya kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awazidishie mara dufu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
AMEN
No comments:
Post a Comment