Wanariadha saba kutoka Cameroon waliokimbia kutoka kijiji cha wanariadha usiku wa manane huenda wanatafuta nyumba mpya au fursa bora za kimichezo ,kwamujibu wa afisa wa olimpiki wa Cameroon.
Miongoni mwao ni wanamasumbwi watano, muogeleaji na mcheza soka mmoja. Wote walikua wameisha hitimisha mashiondano waliyoshiriki.
Sehemu kubwa ya raia milioni 20 wa Cameroon, huzungumza lugha ya Kifaransa na ni miongoni mwa nchi masikini sana duniani.
Tataw alisema pia kuwa wana masumbwi watano pia walikua na vibali vinavyowaruhusu kuzuru Ulaya kwa sababu wana viza ya Schengen kutokana na kua walikua wakifanya mazowezi yao nchini Italia kabla ya mashindano.
Hivyo kutokana na urahisi wa kusafiri kihalali katika mataifa ya Ulaya ikiwemo Ufaransa ambako kuna raia wengi wa Cameroon pamoja na familia za wanariadha hao.
Maofisa wa maandalizi ya Olimpiki ya London wamesema kua ingawa Maofisa wa Cameroon wameomba msaada wa kuwatafuta wanariadha wao, bado hawajavunja sheria yoyote bado viza zao zi hai.
No comments:
Post a Comment