ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 10, 2012

Lipumba afunika Jangwani

 AKIPOKEA KADI  KUTOKA KWA WANACHAMA WAPYA WALIOTOKA CCM 

Chama cha Wananchi (CUF) kimesema licha ya taifa kuwa na rasilimali nyingi kama ardhi na madini mbalimbali wanaonufaika ni matajiri wachache kutokana na kukosekana kwa uongozi imara.

Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema hayo jana katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa operesheni  'Mchakamchaka chinja hadi 2015 tunamaliza.'

Katika operesheni hiyo, CUF inakusudia kutembelea mikoa sita ya  Arusha, Kigoma, Tabora na Kagera na mingine miwili itajulikana baadaye.

Alisema Tanzania ina mapato makubwa lakini hayatumiki katika kukabiliana na umaskini kwa kuwa yanatumika kuwanufaisha wachache kutokana na ukosefu wa uongozi imara,hivyo nchi kurudi nyuma kimaendeleo hali ambayo alisema ni aibu.

Akizungumzia sera ya Kilimo Kwanza alisema inawanufaisha wakulima wakubwa tu kwa kupora ardhi kubwa huku wakulima wadogo wakibakia kama vibarua kinyume cha malengo ya sera ya kuwasaidia wakulima wadogo.

Alisema serikali imekuwa ikiibiwa na watu wachache wakiwemo mawaziri na wakurugenzi kwa kuandaa miradi hewa ya kijanjajanja kwa lengo la kujipatia fedha huku Watanzania wengi wakiendelea kuwa maskini wa kutupwa na baadhi ya vijana kuwa bomu linalotarajiwa kulipuka wakati wowote kutokana na kukosa ajira.

Profesa Lipumba pia alizungumzia mauaji ya Mwandishi wa habari wa Kituo cha Channel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi, akiwa kazini kuwa ni aibu kwa jeshi la polisi na taifa kwa ujumla kwani Tanzania haiko vitani.

Pia alilaaini vikali mauaji hayo na kusema kuwa ni haki ya mwandishi kupata habari bila kubugudhiwa kwa kuwa wao ni daraja muhimu kati ya wananchi matukio yanayotokea nchini.

Naye Haji Duni ambaye pia ni Waziri wa Afya katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar,  alisema anashangazwa na kauli ya Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye, kuwa Jeshi la Polisi linatumia nguvu kubwa kupita kiasi na kuua watu wakati yeye ndiye aliyeasisi polisi kuua raia wakati akiwa madarakani kama waziri mkuu kwa kipindi cha miaka 10 chini ya serikali ya awamu ya tatu.

No comments: