SHIRIKISHO LA NGUMI LA
TAIFA (BFT)
S.L.P 15558
DAR ES SALAAM
September 10, 2012
Email:-bft.tanzania2009@gmail.com
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI.
YAH:-MASHINDANO YA UBINGWA WA TAIFA
17-22/09/2012.
Shirikishi
la ngumi Tanzania (BFT)limeandaa mashindano ya ngumi ya ubingwa wa Taifa 2012
yatakayofanyika kuanzia jumatatu ya tarehe 17-22/09/2012 uwanja wa ndani wa
taifa (indoor stadium) kila siku kuanzia saa 9.00 alasiri.
Awali
mashindano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika kuanzia tarehe 15/09/2012 lakini
kutokana na uwanja wa ndani wa taifa kuwa na shughuri nyingine ya kimichezo ya
ligi ya mpira wa kikapu,sasa mashindano hayo yataanza kutimua vumbi kuanzia
tarehe 17/09/2012.
Lengo la
mashindano hayo ni kupata timu ya taifa ya ngumi yenye sura ya kitaifa
,itakayoshirikisha mikoa yote ya Tanzania bara.ili kuanza maandalizi ya mapema
na ya uhakika kwa ajili ya kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola
2014,mashindano ya Afrika 2015,mashindano ya olimpiki 2016,ubingwa wa dunia na
mashindano mbalimbali tutayopata mwaliko kwa ajili ya kuwakilisha taifa.
Hadi leo jumla ya mikoa kumi na nane (18)
imethibitisha kuja kushiriki katika mashindano hayo,mikoa hiyo ni mikoa ya
kimichezo ya Temeke,Kinondoni na
Ilala.Mingine ni Ngome ya JWTZ,JKT,Magereza na Polisi.Mingine ni
Pwani,Morogoro,Mbeya,Ruvuma,Dodoma,Kigoma,na Bukoba.mikoa mingine ni
Tanga,Arusha ,Tabora na Mwanza.
Uongozi wa
BFT licha ya kutopata udhamini wa uhakika wa kufanikisha mashindano haya,kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali tumejipanga vema kuhakikisha mashindano hayo
yanafanyika kwa kiwango cha hali ya juu ili kufikia lengo la kupata timu ya
taifa kwa wakati kwa maandalizi ya mapema.mashindano hayo yana takiwa kufanyika
kwa bajeti ya milioni ishirini na sita (26,000,000/=).
Sasa Mabadiliko
ya ratiba ya mashindano itakuwa kama ifuatavyo:-
TAREHE
|
MUDA
|
TUKIO
|
16/09/2012
|
|
Timu zote kuwasili dare s salaam.
|
17/09/20123
|
1.00-4.00 Asb
4.00-5.00 Asb
5.00-7.00 Mch
|
Kupima uzito na afya,uwanja wa taifa
wa ndani.
Zoezi la draw na bye na ratiba ya
mashindano.
Semina kwa waamuzi,timu manaja,makocha
kwa ajili ya kupatiwa kanuni na sheria za mashindano.
|
18/09/2012
|
1.00-2.00 Asb
8.00-2.00 Usk
|
Kupima uzito na afya,uwanja wa taifa
wa ndani.
Gwaride la ufunguzi na kuanza
mashindano hatua ya mtoano
|
19/09/2012
|
1.00-2.00 Asb
9.00-2.00 Usk
|
Kupima uzito na afya
Mashindano kuendelea hatua ya mtoano
|
20/09/2012
|
1.00-2.00 Asb
9.00-2.00 Usk
|
Kupima uzito na afya
Mashindano kuendelea kwa hatua ya robo
fainali
|
21/09/2012
|
1.00-2.00 Asb
2.30-8.45Mch
9.00-2.00 Usk
|
Kupima uzito
Mkutano mkuu wa BFT(indoor stadium)
Mashindano kuendelea hatua ya nusu
fainali
|
22/09/2012
|
1.00-2.00 Asb
8.00-2.00 Usk
|
Kupima uzito na afya.
Gwaride la kufunga na kuendelea kwa
mashindano hatua ya fainali.
|
23/09/2012
|
|
Timu zote kuondoka
|
Aidha ajenda
za mkutano mkuu wa wanachama wa bft ni mbili tuambazo ni kupitia na kupitisha
rasmu ya katiba ya BFT na maandalizi ya uchaguzi wa BFT wa kuwapata viongozi
makiniwa kuongoza BFT kwa kipindi cha miaka mine kuanzia marchi 2013 kwa mujibu
wa katiba .
Makore
Mashaga
Katibu Mkuu
BFT.,
Mob:-0713/0784/0763/0773 -58 88 18
Email:-
mashagam@yahoo.om
No comments:
Post a Comment