MOJA KATI YA MAVAZI YALIBINIWA NA PAKA WEAR
KAMPUNI
ya Cat Work Agency imeandaa shoo ya mavazi iliyopewa jina la Green
Carpet Fashion Week ambayo pia itakuwa ni sehemu ya mchakato wa kutafuta
utambulisho wa vazi la taifa.Mwanamitindo na mratibu wa shoo hiyo, Gymkhana Hilal amesema kuwa shoo hiyo itafanyika Desemba, mwaka huu kwenye Hoteli ya Giraffe iliyopo jijini Dar es Salaam na itakuwa ni mwanzo wa utambulisho wa vazi la taifa kwa kuwa baada ya hapo kutakuwa na mradi uliopewa jina la Jakaya Project.
“Kutakuwa na mavazi mbalimbali yatakayoonyeshwa siku hiyo, nipo kwenye mazungumzo na makampuni kadhaa kwa ajili ya udhamini, lakini wanamitindo wanaohitaji kushiriki wanaweza kufika katika ofisi zetu zilizopo Kinondoni Biafra kwa ajili ya kujiandikisha au wanaweza kupata maelezo zaidi kupitia tovuti yetu ya www.pakawear.com
“Mradi wa Jakaya utakuwa umelenga kipindi cha runinga ambacho kitakuwa na mwendelezo kwa kuwa kitakuwa kikirushwa kila wiki, unajua ni ngumu kupata vazi moja liwe la taifa, lakini tunaweza kutengeneza mazingira mazuri ya kuweka utambulisho wa vazi letu,” alisema Gymkhana.
Aliongeza kuwa mpaka sasa ameshabuni mavazi kadhaa kwa ajili ya shoo hiyo yakiwemo mavazi yaliyopewa jina la ‘Hip Hop Swahily style’, mbapo ameanza mazungumzo na makampuni ya nguo ya hapa nchini ikiwa ni sehemu ya kuthamini vitu vya nyumbani.
Gymkhana aliongeza kuwa: “Tumeamua kuipa jina la Jakaya kwa kuwa rais wetu wa sasa Jakaya Kikwete amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia vijana na kuwafungulia njia katika mambo mengi, hivyo hii ni nafasi pekee kwetu kuitumia kuonyesha uzalendo wetu.”
Gymkhana amewahi kubuni mavazi katika amewahi kubuni mavazi katika shoo mbalimbali zikiwemo Swahili Fashion Week, Khanga za Kale Fashion Show na Lady In Red Fashion Show
1 comment:
msipate taabu ya kutafuta vazi la taifa nalo ni KANIKI BARA WATU WALIKUWA WAKIVAA KANINI MNAJIHASHUA BUREEE NA VAZI LENU KANIKI
Post a Comment