ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, October 28, 2012

Shule za New York City, Subway, Amtrack, Mabasi na usafiri wote wa anga kutoka na kuingia Jiji hilo lisilolala umesitishwa  kutokana na Hurricane Sandy ambayo imeanzia Cuba.

Hurricane Sandy inatarajiwa kuanza Jioni ya Leo na kumalizikia Jumatatu asubuhi na watu wengi wameanza kuondoka jiji hilo na watakaobaki wameombwa kukaa ndani ya nyumba zao.

Wakaazi zaidi ya milioni 5 wa New York City hutumia usafiri wa Subway ambayo ni idadi kubwa  na pia mji huu ndio unashikilia rekodi ya kuwa na wasafiri wengi watumiao usafiri wa Treni nchini Marekani na sababu kubwa ni wakaazi wengi wa Jiji hilo sililolala hawamiliki magari.

No comments: