By Pastor Gordon Kalulunga.
*Watatu wajeruhiwa na risasi, wanne wakamatwa..
TAARIFA zilizotufikia hivi punde ni kwamba askari Polisi wanawatawanya wananchi wa Kijiji cha Kamsamba,wilayani Momba mkoani Mbeya kwa ajili ya kumwokoa Mkuu wa wilaya hiyo Abiud SaudeaHali hiyo ilijitokeza kuazia majira ya saa Nane mchana leo baada ya Mkuu hyo wa wilaya kufika kijijini hapo na kuanza kuhutubia huku viongozi hao wa wilaya wakikusudia kumrejesha madarakani Mwenyekiti wa Kijiji hicho Vitus Sauzen aliyetimuliwa kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha.
Hali hiyo iliwakera wananchi na kuanza kuzomea jambo ambalo lilizusha vurugu mbele ya Mkuu huyo wa wilaya, kamanda wa polisi wa wilaya hiyo (OCD) na viongozi wengine.
Kutokana na fujo hizo, askari polisi waliingilia kati
na kuwatawanya wnanchi na mabomu ya machozi hali ambayo haikufua dafu na kuamua
kutumia risasi za moto ambazo zimejeruhi watu watatu ambao wamekimbizwa
Hospitali ya wilaya ya Mbozi mkoani hapa.
Mbali na hao watu wanne wamekamatwa kwa kuhusika na
uratibu wa fujo hizo wakiwemo viongozi wawili wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) katika kata na kijiji hicho cha
Kamsamba.
Waliokamatwa na Polisi ni
pamoja na Richard Nyoni, Michael Simfukwe ambao ni viongozi wa Chadema. Wengine
ni Jofrey Dismas na Sabati Kigaya.
No comments:
Post a Comment