ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 28, 2012

R. I. P CLEMENCE MPEPO "MZEE WA MAKABILA"


CLEMENCE MPEPO "MZEE WA MAKABILA" MTANGAZAJI NA MWANDISHI WA POMBA FM TUTAKUKUMBUKA DAIMA
 DURU za Habari kutoka Mkoani Mbeya zinasema Mtangazaji na Mwandishi Habari wa Redio BOMBA FM Clemence Mpepo amefariki dunia.

Taarifa kutoka chanzo chetu zinasema Mpepo amefariki dunia wakati akipewa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Meneja wa Kituo hicho cha Redio Freddy Herbet imesema ni kweli mpendwa wao amewatoka na juhudi za mazishi zinaendelea kufanyika.Mtangazaji huyo miezi miwili iliyopita alifunga pingu za maisha. Alizaliwa Desemba 17, 1980

Katika fani yake ya Utangazaji alikuwa mahiri kabisa katika Kipindi cha Makabila kilichokuwa kikirushwa katika redio hiyo na hivyo kujizolea umaarufu hata kufikia kuitwa “MZEE WA MAKABILA”

No comments: