ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 4, 2012

Tangazo la sherehe ya kuwakaribisha Balozi Manongi na Naibu wake Ndugu Mwinyi - tarehe 1 December 2012

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania New York na Vitongoji vyake, NYTC (Board na Executive Committee), wanafurahi kuwaalika Watanzania wote wanaoishi New York na Vitongoji vyake, kwenye sherehe ya kuwakaribisha Balozi Manongi na Naibu wake Ndugu Mwinyi, viongozi wapya wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa New York, pia  kumshukuru Dr. Seruhere aliyekuwa Naibu Balozi wa muda na Mlezi wa NYTC.
Sherehe hii itafanyika Jumamosi, tarehe 1 December kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 6 usiku kwenye  ukumbi wa:
Holy Trinity Greek Orthodox Church
10 Mill Road
New Rochelle, NY 10804
Wote mnakaribishwa.
Tunaomba mchango wa dola 25 kutoka kwa kila mtu, na wanafunzi dola 10 kwa ajili ya gharama ya shughuli nzima. Huu mchango upelekwe  kwa wafuatao kabla ya terehe 20 November 2012, Receipts  za mchango zitatolewa .
Miriam Abu (914) 316-2814
Amir Kius (201) 450-5129
Catherine Kyauka (201) 562-2890
Shabani Mseba (347( 712-8539

Tunatanguliza shukrani zetu za dhati.
Uongozi wa NYTC.

No comments: