Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema ajali za ndege zinaweza kuepukika ikiwa marubani watapewa taarifa sahihi kuhusu hali ya anga.
Hayo yalisemwa kijini Dar as Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara ya Uchukuzi, Morrison Mlaki, wakati akiwatunuku vyeti wafanyakazi 33 wa TMA baada ya kupatiwa mafunzo maalum ya taarifa za hali ya hususani ni za anga.
Mlaki alisema elimu wayoipata wafanyakazi hao itawasaidia marubani kujua hali ya anga kama za machafuko ili wachukue hatua mapema wanaoongoza ndege angani.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi, alisema wakufunzi wataboresha huduma za hali ya hewa hasa maeneo ya Ziwa Victoria.
No comments:
Post a Comment