Saturday, December 8, 2012

Dodoma: Mahakama yakabidhi ng’ombe 80 kwa watoto


MAHAKAMA ya Rufaa katika Kanda ya Dodoma, jana iliwapa haki watoto wa marehemu Milika Ndudumizi waliokuwa wamenyang’anywa ng’ombe 82 na mjomba wao na kusisitiza kuwa mifugo hiyo ni mali halali ya watoto hao.
Hata hivyo, mahakama hiyo ilipinga ombi la watoto hao la kutaka kulipwa Sh 20 milioni ,kama gharama za uendeshaji wa kesi hiyo kwa madai kuwa hazikuwa na vielelezo.
Gazeti hili lilikuwa la kwanza kuripoti habari za watoto hao baada ya kupata taarifa kutoka katika Kijiji cha Chipogolo ambako walishakata tamaa kwa madai kuwa mama yao hakuwa mmiliki halali wa mifugo hiyo.
Akisoma hukumu hiyo jana Jaji wa mahakama hiyo, Aisha Kwariko, alisema mahakama imejiridhisha kuwa ng’ombe hao 82 ni mali halali ya marehemu Milika Ndudumizi na hivyo walipaswa kugawiwa watoto wake baada ya yeye kufariki.
Jaji Kwariko alisema kuwa katika kufuatilia kesi hiyo pamoja na ushahidi wa pande zote, ilidhihirika mahakamani hapo kuwa wajomba wa watoto hao hawakuwa na haki ya kuchukua mifugo hiyo.
Mwananchi

1 comment:

ak said...

Hongera sana kaka, nawatakia maisha yenye furaha na amani.