Thursday, December 27, 2012

MH. LAMECK AIRO NA MIKAKATI YAKE KUKUZA ELIMU JIMBO LA RORYA.

Mbunge wa Rorya Lameck Airo akifanya uzinduzi rasmi wa shule ya msingi kata ya Kirogo yenye madarasa mawili tu huku mengine mapya yakiendelea kujengwa kwa nguvu ya wananchi pamoja na sapoti ya mbunge huyo kama sehemu ya kusapoti maendeleo ya elimu wilaya ya Rorya mkoani Mara. 
Hatua yapili kuelekea kuona kibao cha uzinduzi. 
Hatua hii nifaraja kwa wananchi wa kata ya Kirogo kwani ni safari kuelekea kuisaka elimu bora yenye manufaa kwa watoto waishio maeneo ya karibu katani humu.
Jiwe la msingi la jengo hili limewekwa na Mhe. Lameck Airo Mbunge wa Wilaya ya Rorya tarehe 21/12/2012.
Uhaba wa madawati katika shule nyingi za msingi na sekondari nchini umeendelea kuumiza vichwa vya wengi wapenda elimu pamoja na wazazi kwa ujumla hali iliyomlazimu mbunge Lameck Airo kujisukuma kuchangia madawati kama inavyoonekana pichani ndani ya moja ya madarasa haya.
Mara baada ya kufanya ufunguzi kwa shule hiyo Mhe. Mbunge Lameck Airo alizungumza na wananchi wa kata hiyo kuweka msisitizo kwa masuala kadhaa ikiwemo matunzo ya majengo ya shule, ukarabati wa kila mara, kuhamasisha elimu na uboreshaji wa michezo.
Wananchi wa kata ya kirogo wakimsikiliza kwa umakini Mbunge wao kwenye kusanyikohilo.

No comments: