Maggie Munthali (kulia) akiwa na washiriki wengine wakiwakilisha nchi zao Gambia na Burkina Faso
JAMANI HIVI WATANZANIA TUTAACHA LINI KUWA MATAPELI???HUYO DADA "MAGGIE R MUNTHALI"AMEVAA MISS TANZANIA JE MNAMTAMBUA KWAMBA ALIKUWA MISS TANZANIA MWAKA GANI?AU ALISHIRIKI KATIKA MASHINDANO GANI YA KUMTAFUTA MWAKILISHI WA TANZANIA?SISI KAMA WATANZANIA TUMESIKITISHWA SANA NA KUTAPELIWA HUKU.TUMESAHAU KUWA ULIMWENGU HUU WA MITANDAO UONGO UONEKANA MARA MOJA.DADA HUYU ALIONEKANA JUMAMOSI WASHINGTON DC KATIKA MASHINDANO YA KUMTAFUTA MISS AFRICA USA.WASHIRIKI WOTE WALIOSHIRIKI NI WAREMBO WALIOSHINDA MATAJI KATIKA NCHI ZAO WALIZOTOKA....AU WAREMBO WALIOSHINDA MATAJI NDANI YA USA YA KUZIWAKILISHA NCHI ZAO.SASA HUYO DADA HAJAWAHI KUSHIRIKI MISS TANZANIA NA KUSHINDA KULE TANZANIA WALA HAJAWAHI KUSHIRIKI MASHINDANO YA KUMTAFUTA MISS TANZANIA NDANI YA USA...JE IMEKUWAJE AMEVAA UMISS TANZANIA NAKUIWAKILIKSHA TANZANIA JE HASHIM LUNDENGA ANAELEWA SWALA HILI?..JE LUNDENGA ALIMRUHUSU HUYU DADA KUIWAKILISHA TANZANIA NJE YA NCHI?..KAMA ALIMRUHUSU ALITUMIA VIGEZO GANI KUMCHAGUA?..TUNAPENDA KUWAKIRISHA NA TUNAMSAPOTI MTANZANIA YEYOTE ANAYETUWAKIRISHA NJE YA NCHI LAKINI APITIE KATIKA NJIA ZILIZO SAHIHI SIO KUGUSHI KUJIITA MISS TANZANIA WAKATI HAJAWAHI KUSHIRIKI MASHINDANO YOYOTE YA KUTAFUTA MISS TANZANIA NDANI NA NJE YA NCHI?...KAMA TUMEKOSEA ALIISHA WAHI BASI BWANA LUNDENGA TUNAOMBA PICHA ZAKE AKIWA KATIKA MASHINDANO YA KUMTAFUTA MISS TANZANIA POPOTE PALE NDANI NA NJE....NA TUNAOMBA UTWAMBIE JE ALISHINDA NA KUTWAA TAJI HILO?.....WAPO MAMISS WENGI AMBAO WANAFANYA KAZI KUBWA SANA KUWEZA KUFIKIA KUITWA MISS,WAMEVIJA JASHO KUPITIA VIKWAZO HADI KUSHINDA NA KUIWAKIRISHA NCHI VYEMA....TUNAOMBA MTU ANAPOAMUA KUIBEBA BENDERA YA NCHI ASIWE MTU WA KUFOJI.....HUU NI WIZI WA KUMUITA MTU MISS TANZANIA WAKATI HAJAWAHI KUWA..TUNAOMBA PIA SWALA HILI MHESHIMIWA LUNDENGA KAMA SIO LA HALALI BASI LIFIKISHWE KWA WAANDALIZI WA MISS AFRICA USA KWANI INAWEZEKANA KABISA WAMERUBUNIWA..AU LABDA WANAVIGEZO VYAO.TUNAOMBA WATANZANIA MLIOKO NJE YA NCHI MSITUDANGANYE NA KUTUIBIA KWANI WATANZANIA SIKUIZI TUKO KWENYE MITANDAO....HABARI HIIZI PIA TUTAZIPELEKA WIZARA YA MABO YA NJE KWANI HUWEZI KUIWAKIRISHA NCHI PASIPO HALALI..!
AHSANTE.....MUNGU IBARIKI TANZANIA !
Haya ndio Majibu kutoka Miss Tanzania Committee, Tanzania
WADAU WA UREMBO WASHINGTON DC USA...
Salamu kutoka jijini Dar Es Salaam,
Tumesoma maoni yenu kupitia mtandao wa jamii wa Issa Michuzi blogs.com unaohusu taarifa ya mrembo Maggie Munthali kushiriki shindano la urembo la Miss Africa USA.
Mrembo Maggie Munthali alishiriki mashindano ya urembo ya Miss Tanzania Kitongoji cha MZIZIMA mwaka 2005.
Mrembo Maggie alikuwa miongoni wa waliofanikiwa kuingia TOP 3 ya shindano hilo hivyo kupata nafasi ya kuwakilisha kitongoji hicho katika ngazi ya KANDA YA ILALA kwa mwaka huo.
Mrembo huyo hakupata nafasi ya kuingia katika Fainali za Taifa kwa mwaka huo 2005. aliishia ngazi ya Kanda ya Ilala.
Kanda ya Ilala kwa mwaka huo iliwakilishwa na FEZA KESSY, Perminda Raj na LILIAN MUSHI, na mshindi wa mwaka huo alikuwa NANCY SUMARI ambaye pia alitwaa taji la MISS WORLD AFRICA 2005.
Kamati ya Miss Tanzania haina kipingamizi chochote kwa mrembo huyo kushiriki mashindano mengine yoyote ya urembo mahali popote pale.
Kamati inamtakia kila la heri mrembo huyo na wengine watakaojitokeza kutangaza jina la Tanzania katika fani ya urembo.
Hatujui ni vigezo gani walivyotumia hao waandaaji wa shindano hilo la Miss Africa USA, hadi kumpa Jina / sash ya Miss Tanzania, lakini tunaimani tu kwamba ni mrembo anayewakilisha Tanzania japokuwa hakuingia katika Fainali za Taifa.
HIDAN .O. RICCO.
PUBLIC RELATION OFFICER
MISS TANZANIA COMMITTEE
TEL: +255 715 019288
8 comments:
woooooooooooooooooow, just woooooooooooow, interesting, daaaaaaam, thats all i can say, dang!!!!
asante sana kwa ukweli, kwa nini tuna wivu wa maendeleo kwa wanaotangaza nchi yetu nje, jamani ni vema kujiunga na wewe unayeona wivu badala la kuita watu TAPELI.
Haumjui (n) Margaret bwana waulize vizuri nilitamani nijibu before ila nilikuwa nasubiri huo mshushuo huyo aliyeandika na wivu mtoto wa haya na mwezi gogogooooooooooooowatafutie ma mbeleko watasema mengi mwanangu
Mashindano haya yameandaliwa na ni kwa ajili ya African Diaspora wanaoishi US. Hongera Maggie kwa kuingia kwenye Top 20. Kwa maelezo zaidi, pitia www.missAfricaUSA.com. She is beautiful and intelligent girl who needs our support hope she wins.
Maybe she was the only one that was available with a lot of time in her hands.Most Beautiful,Intelligent,young women from Tanzania who are living in America are busy chasing and living their dreams.No one is jealous of her because there's really nothing to be jealous about and i think doing something like this is wonderful for women like her it just comes to show that just because your no longer in your twenties doesn't mean life should stop.So hopefully this title will help her self-esteem.You go girl Keep up the good work.
Wabongo kuchonga midomo jadi yetu,upepo huo utapita.Go Maggie,all da way to the moon if u can,wenye vijiba vya roho poleni. So proud of Maggie,!! Nchi nyingine wamekuja wawili nazaidi,na wamedhaminiwa na communities/Balozi zao. Mtoto wa watu kajigharamia kila kitu mwenyewe,bado twampiga madongo. Damn! Come on people,think b4 u spit/leap!!!!!!!
Keep it up mdogo wangu....KELELE ZA CHURA HAZIMZUII TEMBO KUNYWA MAJI, kwa maana nyingine hizo ni BLESSING, kaza buti huku nyuma tunakuombea na utafikia malengo yako.
Keep it up mdogo wangu....KELELE ZA CHURA HAZIMZUII TEMBO KUNYWA MAJI, kwa maana nyingine hizo ni BLESSING, kaza buti huku nyuma tunakuombea na utafikia malengo yako.
Post a Comment