ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 31, 2012

MPAMBANO WA MASUMBWI KUPIGWA Janual 27 katika ukumbi wa CCM Tandare


Mabondia Hassan Mandulla na Jems Martin wanatarajia kupanda ulingoni Janual 27 katika ukumbi wa wa CCM Tandare Dar es salaam akizungumza mpambano huo mwandaaji Waziri Rosta 

amesema kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi yakiwemo ya mabondia maarufu na chipkizi alisema mapambano ya utangulizi ni Fadhiri Majia na Anton Matiasi mpambano mwingine

Utawakutanisha Shabani Kilumbelumbe na Mwaite Juma na Chaeles Mashali atavaana na Adam Ngange, Julias Noro atapambana na Abdallah Luwaje   mpambano mwingine utawakutanisha Rajabu Tumaini na Daudi Anton na Rashid Mohamed Atavaana na Eliman Richard wakati Rashid Hamisi atamvaa Omary Shabani

Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio,Juan Emanuel Marquez, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina.

 michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema.


 Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo. 


Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana

No comments: