Mwanadada raia wa Kenya aliyekuwa akiishi na kufanya kazi Manchester nchini Uingereza amejiua kutokana na upweke uliokuwa ukimkabili.Marehemu aliyefahamika kwa jina la Sharon Bukokhe alikuwa ni sales manager wa mradi wa family planning kwa nchi za dunia ya tatu.
Akiwa anaishi Uingereza mwenyewe toka 2002,mume wake akisoma na kuishi nchini Afrika ya Kusini,mama yake akiishi Virginia Marekani,dada yake akiishi Canada..Ndugu pekee aliyekuwa Uingereza ni kaka yake lakini ni mbali sana na alipokuwa akiishi yeye.Jambo ambalo lilimpa upweke sana na kuamua kujiua.Marafiki aliokuwa akiishi nao wanasema alikuwa ni mtu mwenye furaha,akili na mbunifu kiasi amabcho ilikuwa ngumu kujua kama angeweza kufikia hatua hiyo.Mara nyingi alikuwa akisikika kusema ana upweke na anaimiss familia yake na mumewe.
Sharon Bukokhe aliyekuwa na miaka 28 kabla ya kujiua alifanya utafiti wa njia mbali mbali za kujiua kupitia laptop yake.Laptop ilikutwa ndani kwake mlango ulipovunjwa na mwili kukutwa chini.Kabla ya kujiua alijiremba,akapaka rangi ya kucha na kuvaa vizuri kama mtu anayeenda kwenye mtoko flani kisha akajimaliza.
Kwasababu hiyo hiyo ya upweke aliwahi kugundulika anaugonjwa unaoitwa bipolar disorder.Ugonjwa huu unakufanya uwe na mood swing ambazo ni dalili ya ugonjwa wa msongo mawazo(depression). (Habari kwa hisani ya Dina Morios)
1 comment:
upweke si mchezo mimi mwenyewe nina upweke hivi sasa zamani nilifikiria kujiuwa lakin sasa hivi sina fikra hizi ila naina upwekwe wa hali ya juu na niko single
Post a Comment