KIKOSI
cha wachezaji 27 wa Yanga Sc kinatarajiwa kuondoka nchini usiku wa
jumamosi kuelekea nchini uturuki kwa ajili ya kuweka kambi maalum ya
kujiandaa na mashindano mbalimbali.
Mwenyekiti
wa kamati ya Mashindano na mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Yanga,
Abdallah Binkleb ameiambia Sports Lady maandalizi ya safari hiyo
yamekamilika na kwamba wachezaji watakaokwenda huko pamoja na viongozi
watajulikana kesho.
Amesema
kwamba kambi hiyo itakisaidia sana kikosi katika maandalizi yake ya
mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom pamoja na michuano ya Kagame
itakayofanyika Kigali, Rwanda ambapo Yanga ni bingwa tetezi.
"Ndo
maana tumetaka kwenda Uturuki kwani huko kuna facilities nzuri kwa
ajili ya kambi...pia huko tunataraji kiucheza mechi kadhaa za
kirafiki,"amesema.
Yanga
inayonolewa na Ernie Brandts jana ilichapwa bao 1-0 na mabingwa wa soka
nchini Kenya, Tusker Fc katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment