Kikosi cha Zanzibar Heroes kilichocheza mechi ya Kombe la Chalenji dhidi ya Burundi katika hatua ya robo fainali
Wachezaji wa Zanzibar Heroes wakimbeba kocha wa Salum Bausi baada ya kutwaa ushindi wa tatu kufuatia kuifunga Tanzania Bara kwa matuta 6-5
Beki wa timu ya Zanzibar Heroes, Haroub Nadir akimzuia mshambuliaji wa trimu ya Zanzibar Heroes, John Boko wakati wa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela nchini Uganda
Mchezaji wa timu ya Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager,Athuman Chuji akimtoka beki wa timu ya Zanzibar Heroes, Sabri Alliy Makame wakati wa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu katika michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa Nelson Mandela nchini Uganda jana
NAHODHA wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ni miongoni mwa wachezaji 16 waliofungiwa kwa muda usiojulikana kucheza soka popote duniani na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), ambacho pia kimeivunja rasmi timu ya taifa, Zanzibar Heroes kwa tuhuma ya utovu wa nidhamu.
Akitangaza maamuzi ya kikao cha Kamati Utendaji ya ZFA kilichofanyika leo mchana kwenye ofisi za chama hicho zilizopo Kiembe Samaki, nje kidogo ya mji wa Zanzibar, Makamu wa Rais wa ZFA Unguja, Alhaj Haji Ameir, alisema wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji waliohudhuria kikao wameunga mkono hatua hiyo ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine.
Kikao hicho cha dharura kimekuja kufuatia sakata la wachezaji wa Zanzibar Heroes kuamua kugawana kiasi cha dola za Kimarekani 10,000 walizopata baada ya kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Chalenji) iliyomalizika wiki iliyopita mjini Kampala, Uganda, kufuatia kuifunga Kilimanjaro Stars ta Tanzania Bara kwa penalti 6-5, baada ya sare ya 1-1.
Inadaiwa kuwa wachezaji hao waliamua kugawana fedha hizo kwa madai kuwa wamekuwa wakidhulumiwa fedha zao na ZFA.
Hata hivyo, katika ufafanuzi uliotolewa leo na Katibu Mkuu wa ZFA Taifa, Kassim Haji Salum, haijawahi kutokea wachezaji wa timu hiyo kudhulumiwa haki yao akikumbushia fedha za zawadi walizopata mwaka 1995 katika mashindano kama hayo yaliyofanyika nchini Uganda na Zanzibar ikafanikiwa kutwaa ubingwa na mwaka 2009 waliposhika nafasi ya tatu kwamba mara zote walipewa stahili zao.
Kwa upande wake, kocha wa Zanzibar, Salum Bausi ambaye alitangaza rasmi kujiuzulu kuifundisha timu hiyo, alisema hatua hiyo ni sahihi kabisa kwa sababu kitendo hicho kimewafedhehesha wadau wa soka na Wazanzibari kwa ujumla.
Tayari ZFA Taifa walishatuma barua rasmi kwa TFF juu ya hatua hiyo huku nakala ya barua hizo zikitarajiwa kusambazwa kwa klabu wanazochezea wachezaji hao.
Wachezaji wanne walionusurika na adhabu hiyo ni wale walioamua kuzirejesha fedha hizo ambao majina yao hayakutajwa kwa sababu maalum, hata hivyo taarifa zilizopo ni kuwa wachezaji hao wanatoka katika klabu ya Kipanga timu inayomilikiwa na JWTZ, Jamhuri, Zimamoto na KMKM.
Kikosi cha Zanzibar kilichokwenda kwenye Chalenji ni makipa; Mwadini Ali (Azam), Suleiman Hamad (Black Sella), Abdalla Juma (Kipanga), mabeki; Nassor Masoud 'Chollo' (Simba), Samir Haji Nuhu (Azam), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub Ali 'Canavaro' (Yanga), Aziz Said Ali (KMkM), Mohammed Juma Azan (JKU) na Ali Mohammed Seif (Mtende Rangers).
Viungo ni; Hamad Mshamata (Chuoni), Ali Bakar (Mtende Rangers), Is-haka Mohammed (JKU), Twaha Mohammed (Mtibwa Sugar), Suleiman Kassim 'Selembe' (Coastal Union), Saad Ali Makame (Zanzibar All Stars), Makame Gozi (Zimamoto), Issa Othman Ali (Miembeni), Aleyuu Saleh (Black Sella), Khamis Mcha Khamis 'Viali' (Azam) na washambuliaji, Amir Hamad (JKT Oljoro), Jaku Juma Jaku (Mafunzo), Abdallah Othman (Jamhuri), Nassor Juma (JKU) na Faki Mwalim (Chipukizi).
4 comments:
Kila mwanadamu hakosi wema . Ni kweli utovu wa nidhamu lakina NAIOMBA ZANZIBAR YOTE kwa la leo MUWASAMEHE......kiuchumi na kiutamaduni bora tuwasamehe kwa karipio kali; lakini VIPAJI tusiviue VIPAJI.
SITAKI NISEME ZAIDI....tusiue vipaji kwa dola alfu kumi
Sitaki sitaki sitaki wapewe karipio kali mno......wawe wavumilivu....wasiwe waroho....na uongozi nao ujifunze kwa hilo NAO.....WASIWE WAROHO.
Vipaji tusiviue. Tunadai FIFA tutaanzia wapi? tunaanza sasa.
Maalim Khamis Mussa , Bausi mwenyewe na Suleiman bin Jabir mumecheza mipira na mnafahamu fika ugumu wa kuvikuza vipaji zanzibar.
Tutajuta saaaaaaaana.Wamefanya makosa lakini tuwasamehe , sikufurahishwa na walilofanya
ZFA kuweni na hekima kidogo. vijana kweli wamekosa hilo halina mjadala. Ila sidhani kama adhabu iliyototewa ni relavant na kosa lao kwa manufaa ya mpira wa zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Walipaswa wapewe Onyo kali kwa tendo walilofanya Ila kuwasimamisha wote kucheza mpira popote ni Kukurupuka. Hii inathibitisha jinsi viongozi wasivyo makini na na watu wa kutoa maamuzi ya jazba. Kuna tatizo hata kwenye Chama cha soka Zanzibar ndio maana hata jambo kama hilo limeweza kutokea. Vijana wamekosa Imani kwa Viongozi wao, tumeona suala la msemajina Katibu wa ZFA. Yote yanaonesha udhaifu mkubwa kwa uongozi wa Makungu. Hivi Lipi kosa kubwa kati ya kugawana fedha za zawadi na Kuitaka timu icheze chini ya kiwango katika kombe la Mapinduzi ili timu kumbwa iweze kuendelea na mashindano na kupata mapato makubwa?
ni jambo la muhimu kujiuliza kwa nini wanafanya hivi hawa wachezaji wetu. nidhamu ni kitu cha muhimu si katika michezo tu bali katika uendeshaji wa jambo lolote lile. iwapo kwa kisingizio sababu za kiuchumi ndio hawa wachezaji wakaamua kufanya hivi hilo halikubaliki,huo ni uhuni na hata kama mtoto wako wa kumzaa atakosa adabu ni lazima kumuadibisha. maadili yamepotea sana zanzibar, nasema zanzibar kwa sababu ndiko nilikotoka.vijana hawa waamuriwe kurudisha fedha zote mara moja, na watakao kaidi amri waadhibiwe kwa adhabu kubwa ili iwe fundisho kwa wengine.watakaorudisha wasamehewe kwa karipio kali, hali kadhalika kama itagundulika madai yao ya kudhulumiwa ni ya kweli basi na waliowadhulumu pia waadhibiwe kwa adhabu kali. asante tudumishe nidhamu.
Ni sawa Vijana wamekosea na wanastahili adhabu. ila ipo haja ya kuangalia Intergrity ya viongozi wa soka nao. Hao viongozi wetu wameonesha udhaifu mkubwa katika utendaji wao ndio maana hili likatokea. Angalia maamuzi ya kiubabaishaji yanayofanywa nakamati ya utendaji namwenyekiti wa ZFA. Angalia kigeugeu cha fainali ya kombe la ujirani mwema. angali mashindano ya kombe la mapinduzi waakati Viongozi hawa walipowataka wazanzibari kuifungish timu ili simba iingie fainali na hatimae waweze mkupata mapoato zaidi hali iliyopelekea Bausi kujiuzuli. Viongezi nao wapo after money ndio maana vijana wakakosa imani nao.
Post a Comment