ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 31, 2013

ASKARI POLISI NA MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA MWANGOSI WAKIMBIA CHUMBA CHA MAHAKAMA ,HAKIMU AGEUKA MBOGO

Hapa mtuhumiwa huyo akikimbiziwa mahabusu ili kukwepa picha ya wanahabari 
Hapa akiingizwa mahakamani 

 
 wanahabari wa radio nuru Fm wakifanya mawasiliano kujua mtuhumiwa huyo kama amefikishwa mahakamani ama bado ,hii ilikuwa mida ya saa 4 asubuhi kabla ya mahakama hiyo kuanza 
Na Francis Godwin
SAKATA la mtuhumiwa wa mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi limezidi kuchukua sura mpya baada ya askari waliomfikisha mtuhumiwa huyo wa mauaji askari wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) kumtibua hakimu na kuageza mtuhumiwa huyo kurudishwa tena kizimbani kwa kudharau mahakama hiyo.

Tukio hilo lilitokea leo majira ya saa5.35 kwa askari hao watatu ambao majina yao hayakuweza kufahamika mara moja kumshusha kizimbani mtuhumiwa huyo wa mauwaji na kumkimbizia mahabusu kama njia ya kukwepa kupigwa picha na wanahabari waliokuwepo hapo lilitokea mara baada ya mahakama hiyo kuombwa kutaja tarehe nyingine ya kutajwa kesi hiyo.

Huku bado mahakama ikiwa inaendelea kwa hakimu kutaja tarehe ya kesi hiyo namba ya mauwaji kesi namba 1 ya mwaka 2012 mtuhumiwa wa mauwaji alishuka kizimbani huku akivaa kofia yake ya sweta (mzula)na miwani ya giza na kuanza kushuka jukwaani kabla ya hakimu kumtaka mtuhumiwa huyo kutovalia kofia hiyo kizimbani huku kabla ya mahakama kumalizika.

Wakati hakimu huyo akijiandaa kusimama ili kuhitimisha shughuli za kimahakama kwa siku hiyo ghafla alijikuta anabaki na mwanasheria wa mahakama ,kalani wake ,wanahabari ,askari mmoja na ndugu wawili wa mtuhumiwa huyo huku askari watatu wenye silaha na mtuhumiwa huyo wakiwa tayari wameondoka ndani ya chumba cha mahakama hiyo.

“Mbona hao askari wanamtoa mtuhumiwa bila utaratibu wa mahakama hebu mwanasheria waambie wamrudishe ndani mtuhumiwa ....huu si utaratibu mbona wanafanya fujo mahakamani hao” alisikika akisemahakimu mkazi wilaya ya Iringa Dyness Lyimo

Hata hivyo pamoja na jitihada za mwanasheria wa serikali Adolf Maganda kuwaita kwa sauti askari hao kuwataka kumrudisha ndani ya mahakama mtuhumiwa huyo bado askari hao walizidi kukimbia na mtuhumiwa kwenda nae mahabusu na baada ya dakika kama 5 hivi ndipo mwanasheria huyo aliporejea na askari hao na mtuhumiwa ambae hata hivyo hakwenda kusimama kizimbani na badala yake alikwenda upande wa kushoto wa mahakama hiyo ambako alikuwa amekaa mwanzoni kabla ya mahakama kuanza na kuketi katika kiti huku akiwa amevaa miwani na kofia yake.

Kutoka na tukio hilo hakimu huyo alilazimika kuwahoji askari hao watatu kwa vurugu hizo walizozifanya kwa kuwauliza swali moja pekee kuwa wanaona walichofanya ni sahihi na askari hao kuomba msahama kuwa samahani mheshimiwa.

Mwendesha mashtaka wa jamhuri Adolf Maganda aliiomba mahakama hiyo kutaja tarehe nyingine ya kutajwa tena kesi hiyo ambayo ilitajwa Januari 27 na mtuhumiwa huyo kushindwa kufika kutokana na tatizo la ugonjwa lililokuwa likimsumbua .

Hata hivyo mahakamani hiyo liahirisha kesi hiyo hadi Februari 14 mwaka huu kesi hiyo itakapofikishwa mahakani hapo kwa kutajwa tena.

Mtuhumiwa huyo anatuhumiwa kumuua kwa bomu aliyekuwa mwandishi wa habari wa Chanel Tena mkoa wa Iringa marehemu Mwangosi septemba 2 Septemba mwaka jana katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa wakati wa vurugu kati ya polisi na wafuasi wa Chadema .kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai. Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002,

No comments: