Mke wa Naibu Spika wa Bunge la la Korea Kusini, Bi. Han Myeong-Hee, akivishwa zawadi ya kidani na Bw. Martin Malim (kushoto), wakati alipotembelea Chuo cha Elimu ya Ufundi Stadi (VETA) cha Kipawa, Dar es Salaam. Picha na Prona Mumwi
Madereva na abiria wakiyaangalia magari, mara baada ya kugongana eneo la Mtoni Msikitini Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam. Uzembe wa baadhi ya madereva unasababisha ajali zinazochangia madhara kwa abiria na uharibifu wa mali. (Picha na Charles Lucas)
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara (kushoto), akipiga mpira kama ishara ya uzinduzi wa mashindano ya Kombe la Meya katika uzinduzi uliofanyika Kinondoni, Dar es Salaam juzi.Kulia ni Meya wa manispaa hiyo, Yusuph Mwenda.Picha na Peter Twite
Msukuma mkokoteni akisafirisha sanduku za chuma kwa ajili ya maandalizi ya kuuza kama alivyokutwa mtaa wa msimbazi Dar es Salaam. Sanduku hizo hutumika hasa kwa wanafunzi wa shule.Picha na Prona Mumwi
Mkazi wa jijini akipanda gari kwa kuingilia dirishani, kwenye gari namba T 288 AZB linalo fanya ruti kati ya madafu Kariakoo, kama alivyo kutwa na mpiga picha wetu Dar es Salaam. Abiria wamekuwa kero kwa makonda kutokana na uharibifu wa kuvunjwa vioo vya madirisha.Picha na Prona Mumwi
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya timu ya Yanga, Abdallah Bin Kleb akimkabidhi bahasha yenye fedha taslimu sh. mil 1 beki wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa (kulia) wakati wa Mkutano Mkuu wa kila mwaka uliofanyika katika Ukumbi wa Bwalo na Polisi, Oysterbay Dar es Salaam.Na Mpigapicha Wetu
No comments:
Post a Comment