Ujenzi wa mji mpya wa Magomeni unatarajiwa kuanza Februari mwaka huu, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya Manispaa ya Kinondoni na wawekezaji.
Akizungumza na NIPASHE jana Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Fortunatus Fwema, alisema wanatarajia kukutana na wawekezaji Januari 30, mwaka huu kwa ajili ya mazungumzo kabla ya kuanza ujenzi huo.
“Tulitangaza tenda ya kupata wawekezaji wa kujenga mji mpya wa Magomeni ambao utajengwa kwa ploti za aina tatu, za biashara, nyumba za kuishi na ofisi,” alisema Fwema na kuongeza:
“Kila ploti tumechagua wawekezaji sita na tutafanya nao mazungumzo kabla ya kuanza ujenzi, kuna masharti tutakayowapa endapo watakubaliana nayo tunaamini ujenzi unaweza kuanza Februari mwaka huu.”
No comments:
Post a Comment