Makamu wa rais wa UTPC Jane Mihanjo akimkabidhi mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Lindi Abdulaziz Ahmeidvitendea kazi kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa UTPC Bw Karsan.
Kamera za Kisasa kabisa.
Muungano wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania umetoa vifaa vya kazi (vitendea kazi) vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 35 kwa kila klabu ya wanahabari Mikoani kwa lengo la kuboresha utendaji kazi, weledi na kujenga uchumi wa vilabu hivyo,wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Lindi jana.
Makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za Dar City Press Club, vifaa ambavyo ni pamoja na kamera, KOMPYUTA,Runinga na zana za kisasa za mikutano na semina (projector) Ikiwemo machine yakopi(Photocopy),Makamu wa Rais wa UTPC,Bi Jane Mihanji alimkabidhi vifaa hivyo Mwenyekiti wa Lindi Press club,Abdulaziz Ahmeid na amehimiza utunzaji wa zana hizo pamoja na nidhamu ya matumizi ili kukomboa waandishi Mikoani ikiwemo kujiongezea kipato.
No comments:
Post a Comment